Kiongozi machachari wa vijana Afrika Kusini, Julius Malema ameshindwa rufani yake kupinga kuenguliwa kwenye chama cha Africa National Congress (ANC). Jopo la rufani lililokaa jana usiku lilibariki uamuzi wa ANC uliofikiwa Novemba mwaka jana wa kumuengua Malema kwenye kiti cha Urais wa Vijana wa chama hicho kwa miaka mitano baada ya kumtia hatiani kwa uchochezi dhidi ya viongozi wa chama hicho.
Uamuzi huo ni pigo kwa Malema, mwenye umri wa miaka 30, katika harakati zake za kisiasa ambapo kwa kipindi kirefu amekuwa chanzo cha migogoro ndani ya chama hicho kutokana na mitazamo yake ndani ya ANC. Malema pia atachunguzwa akaunti zake.
Baada ya hukumu hiyo, inasemekana viongozi wa chama hicho walitoa fursa nyingine kwa Malema kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
No comments:
Post a Comment