Monday, March 19, 2012

MAJENGO HAYA KWA BARABARA ZIPI HASA?

 DAR ES SALAAM YAPENDEZA!!  Hili ni moja ya majengo marefu yanayoendelea kujengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam maeneo ya Posta. Lakini jambo la kujiuliza, "Kwa barabara zipi hasa?" Najiuliza hivyo kwa kuzingatia kwamba wengi wa wapangaji wa majengo haya wanatokea nje ya mji ambako miundombinu ni mibovu mno hasa barabara ambako foleni imekithiri kuingia mjini. Je, haya ni maendeleo ama tatizo jipya? Ushauri wa bure: Haya majengo yangejengwa nje ya jiji maeneo kama ya Mwenge, Tegeta, Ubungo, Kimara na kwingineko. (Picha na ziro99blog)

No comments: