Baada ya tetesi zilizoripotiwa juzi, sasa mahusiano ya kimapenzi kati ya Binti wa Whitney Houston, Bobbi Kristina na kaka yake wa kufikia, Nick yamewekwa hadharani baada ya wawili hao kuonekana wakikata mitaa huku kukiwa na ishara zote za kuwa wapenzi kama walivyonaswa kwenye video hapo juu. Imeripotiwa kwamba habari hizo zimepokelewa kwa hisia tofauti na bibi yake, Cissy Houston, mama wa Whitney, ambaye amesema kinachofanyika ni uchafu wa hali ya juu na pengine 'doa' kwa familia hiyo. Mama huyo alifika mbali zaidi kwa kusema, "Nick anamganda Bobbi akitaka afaidi mali ambazo binti huyo amerithishwa na mama yake, hakuna cha zaidi." Aliendelea kusema kwamba ni marufuku kijana huyo kukanyaga kwenye nyumba iliyoachwa na Whitney Houston kwa kuwa hawamtambui. Lakini pamoja na hayo yote zimevuja habari kwamba Bobbi tayari amevishwa pete ya uchumba (kama anayoonekana pichani chini) na kijana huyo na kwamba aliwaambia rafiki zake wa karibu, "Hakuna mtu ninayemuamini katika dunia hii kama Nick, yeye ni kila kitu kwangu."

No comments:
Post a Comment