Tuesday, March 27, 2012

KIZUIZI HIKI UTATA MTUPU...

Kizuizi cha magari katika geti lililoko jirani na Chuo cha Ardhi, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa tangazo linaloonekana kushoto, ni kwamba kila gari linalopita hapo hutakiwa kusimama kwa ukaguzi. Hali ilikuwa tofauti asubuhi hii ambapo askari waliokuwapo walikuwa wakiruhusu magari bila kukagua chochote. Kama hali ni hivyo geti hilo la nini sasa kama si kero tu kwa madereva na watumiaji wa barabara hiyo? (Picha na ziro99blog)

No comments: