Monday, March 26, 2012

KALI ZAZIDI KURINDIMA DAWA ZA KULEVYA ZA WHITNEY...

PICHA JUU KUSHOTO: Ray J. CHINI: Leolah Brown JUU KULIA: Hoteli ya Beverly Hills kilipotokea kifo cha Whitney. CHINI: Bafu alimoanguka na kuzama Whitney (picha ndogo).

Imeelezwa kuwa mtu aliyekuwa akimuuzia dawa za kulevya Whitney Houston alisomba ushahidi wote wa dawa hizo kwenye chumba baada ya kuona ameanguka na kuzama bafuni, ripoti zimeweka hadharani.
Ofisi ya Mkemia Mkuu imethibitisha kuwa Whitney alitumia dawa hizo ‘japo kwa kiwango kidogo kabla hajaanguka bafuni.’
Lakini hakuna hata chembe moja ya dawa hizo iliyokutwa chumbani kwake kwenye hoteli hiyo wakati wapelelezi walipopekua na inasemekana pia hata mashuka hayakukutwa.
Imedaiwa kuwa Jeshi la Polisi mjini Beverly Hills bado hawajafunga jalada la kesi hiyo na kwamba wanaendelea kupeleleza sasa kama kesi ya kujaribu kupoteza ushahidi.
Wameongeza kwamba: “Chanzo kimoja ambacho kiko karibu mno na tukio hilo kimetuambia, mtu aliyeziondoa dawa hizo chumbani ndiye pia aliyemletea Whitney.”
Wakati huohuo mpenzi wa Whitney waliyekuwa wakiachana na kurudiana mara kadhaa amekanusha vikali tuhuma za kwamba alikuwa akipeleka dawa za kulevya kwa Whitney, zilizoelekezwa kwake kutoka kwa dada wa Bobby Brown, Leolah Brown.
Msemaji wa mpenzi huyo wa Whitney  ametupilia mbali tuhuma hizo za Leolah wakati alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha HLN’s Dr. Drew kwamba Ray J amechangia kifo chake kwamba dawa alizompeleka hotelini ndio chanzo cha maafa hayo Februari 11, kwamba ni taarifa za uongo.
Lakini mdogo wa Ray J amemtetea kaka yake kwa kusema: “Kaka alikuwa hata hajui kama Whitney amerudi kutumia dawa za kulevya.”

No comments: