Monday, March 26, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mahojiano kati ya baba na mtoto makini yalinaswa kama ifuatavyo. BABA: Hebu niletee soda. MTOTO: Pepsi au Coca?  BABA: Pepsi  MTOTO: Ya chupa au kopo? BABA: Ya kopo MTOTO: Ya baridi au ya moto? BABA: Hee, mbona maswali mengi, basi niletee maji MTOTO: Ya hapa nyumbani au dukani? BABA: Ya hapa MTOTO: Ya baridi au moto? BABA: Ya baridi MTOTO: Kwenye glasi au kikombe? BABA: Hebu kalete kabla sijakupiga na ufagio MTOTO: Wa chelewa au nyasi? BABA: Ntakuua we motto MTOTO: utanichoma kisu au utanipiga bastola? BABA: Na bastola MTOTO: Kichwani au tumboni? BABA: Kichwani, nimekwambia toka nje MTOTO: sasa hivi au baadae BABA: Sasa hivi MTOTO: Maji hutaki tena? BABA: Ngoja utanitambua. Mtoto akatoka nduki huyooooo!

No comments: