Friday, March 30, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mzazi mmoja anamfokea mwanae akimtaka aende kulala. Lakini katika hali isiyo ya kawaida yule mtoto akawa anataka kumuomba kitu mzazi wake ambaye wakati huo hakutaka kabisa kusikiliza. Majibizano yao yalikuwa hivi…BABA: Nimekwambia Faraji nenda kalale. MTOTO: Sawa baba, lakini naomba unipe maji ya kunywa. BABA: Sikupi, nasema kalale. MTOTO: Sawa, lakini nipe maji ya kunywa. BABA: Nimesema kalale kabla sijaenda kuchukua kiboko. MTOTO: Sawa, ukichukua kiboko usisahau na maji. BABA: Nasema nitakutandika wewe! MTOTO: Ukishanitandika unipe na maji!! Duh, mzazi ikabidi awe mpole…

No comments: