Saturday, March 17, 2012
CHEKA TARATIBU...
Mlevi mmoja akiwa kasinzia ndani ya gari lake kwenye taa za kuongozea magari pale TAZARA, Dar es Salaam, ghafla akagutushwa na askari wa doria aliyekuwa akigonga kwenye kioo cha gari lake. Baada ya kuhojiwa kwa muda yule jamaa akagundua kwamba yule askari alikuwa akimtuhumu kwa ulevi. Ili kutaka kuepuka soo jamaa akamwomba yule askari apande kwenye gari aende naye hadi kwake ili athibitishe kuwa hajalewa kama anavyodhani. Askari akakubali na safari kuelekea maeneo ya Tabata Mawenzi ikaanza. Bahati mbaya kutokana na kilevi, jamaa yule akapaki gari nyumba ya jirani badala ya kwake. Akamwambia yule askari, "Haya karibu kwangu ndio hapa." Wakashuka na kuelekea ndani ambapo sebuleni wakakuta watoto wakitazama tamthilia ya Maudodo. "Afande hawa unaowaona ni wanangu," alitambulisha yule mlevi. Hatua kadhaa jikoni wakakuta binti akipika, "Afande huyu ni hausigeli wetu." Akaelekea chumbani na kukuta watu wawili wamelala kitandani, "Afande yule pale ni mke wangu." Kwa mshangao afande akauliza, "Na yule mwanaume ni nani?" Mlevi akajibu, "Ooh acha papara afande, yule ni mimi." Duh, kweli ulevi noma!!!
This is a blog that brings you hot news that aims to educate the community about various things including sports, culture, art, entertainment and social. This blog does not involve political issues at all. We ask for your cooperation and to contribute opinions on the various information we bring to you.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment