Wanandoa wawili wakiwa kwenye mapumziko yao, mume akaomba atenge droo moja kwa ajili ya matumizi yake binafsi ambalo mkewe hatalifungua. Mke akakubali. Baada ya miaka 30 ya ndoa yao, mke akagundua lile droo limeachwa wazi. Akachungulia ndani na kuona mipira mitatu ya kuchezea gofu na Shilingi elfu kumi. Mume aliporejea kutoka kazini, mke akamvamia na kutaka apewe maelezo juu ya vile alivyovikuta kwenye droo. Bila wasiwasi mume akajibu, "Kila nilipoisaliti ndoa yetu niliweka mpira mmoja kwenye droo." Mke akatafakari kwa miaka yote 30 ina maana mume kamsaliti mara tatu tu akajipa moyo kuwa sio mbaya. Kisha akauliza tena, "Lakini pia nimekuta elfu kumi ndani." Mume akajibu, "Kila ilipofikia mipira kumi nilikuwa nauza." Duh, ndoa hizi!!

No comments:
Post a Comment