Picha tofauti zinamuonesha Bobbi Brown akiwa kwenye mishemishe mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Los Angeles. Kushoto akisubiri basi na mpenzi wake Alicia. Katikati (juu) wanaonekana wakishusha mizigo yao tayari kupanda basi (chini). Kulia anaonekana akikokota mizigo yake kuelekea kwenye basi.
Aliyekuwa mume wa mwanamuziki Whitney Houston, Bobby Brown imeelezwa kwamba sasa yuko kwenye hali mbaya sana kifedha kwa lugha rahisi ‘kafulia’.
Bobby ambaye alivuna fedha nyingi sana katika mauzo ya albamu yake iliyotamba katika miaka ya 1980 ya “Don't Be Cruel” ameonekana kuwa katika hali ngumu hadi kufikia kutumia usafiri wa mabasi maalumu ya Uwanja wa Ndege wa Los Angeles jana. Usafiri huo hutumiwa zaidi na watu wa daraja ya kawaida nchini humo.
Mwimbaji huyo maarufu wa miondoko ya RnB, alinaswa akikokota mizigo yake mara baada ya kuwasili uwanjani hapo akiambatana na mpenzi wake wa sasa, Alicia Etheridge hali iliyozidi kutia mashaka kwamba hata pesa ya kuwalipa wapagazi ilikuwa tatizo.
Haikushangaza pale gwiji huyo wa zamani mwenye miaka 43 alipoonekana akielekea kupanda basi hilo kupata jibu kwamba amekuwa kwenye matatizo ya kifedha.
Imeelezwa mapema wiki hii kwamba Bobby aliomba mahakamani kuwa vifaa na mali ambazo alikuwa akizimiliki kwa pamoja na Whitney zilizokuwa zikihifadhiwa zipigwe mnada sababu hawezi kumudu kulipia gharama za uhifadhi.
Katika hati ya kiapo aliyowasilisha mahakamani hapo wakati wa kutalikiana mwaka 2007, alisema wanandoa hao wanakabiliwa na hofu ya kufilisika.
Alisema, “Hakuna siri kwamba mimi (na Whitney pia) tuna majukumu yanayohitaji pesa ambayo hatuwezi kumudu.”
“Mwaka mmoja tu baada ya kuachana, mali zetu zilizoshikiliwa zilipigwa mnada kutokana na hukumu ya kesi ya kushindwa kulipia malimbikizo ya gharama za uhifadhi,” aliongeza Bobby.
Aliendelea, “Kwa kuongezea, baada ya kuachana na Whitney sikuwa na pa kwenda na nilikuwa na pesa kidogo tu mkononi. Kwa kifupi nilikuwa sina makazi.”
Na matatizo ya kifedha si tatizo pekee linalomuumiza kichwa nyota huyo kwa sasa kwani hatua ya binti yake Bobbi Kristina Brown aliyezaa na Whitney kutaka kutumia jina la ukoo wa Houston badala ya Brown, inazidi kutia chumvi kwenye majeraha.
Katika wosia wake, Whitney alimrithisha binti yake huyo jumba lake la kifahari huku akimuacha mume wake huyo wa zamani mikono mitupu.

No comments:
Post a Comment