Saturday, March 10, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mvutaji sigara kazunguka kila kona ya mtaa fulani maeneo ya Chanika bila kuona duka ambako angeweza kupata sigara. Hatua chache mbele kakutana na mtoto mmoja na bila simile akamsimamisha, "Hujambo kijana, eti hapa duka liko wapi?" Yule mtoto akajibu, "Mh, hata sijui." Jamaa akaachana naye na kuendelea kutafuta duka. Baada ya hatua kadhaa akasikia sauti ya yule mtoto ikimwita kwa nyuma. Jamaa akasimama huku akiwa na imani kwamba mtoto amekumbuka lilipo duka, "Enhe, unasemaje?" Yule mtoto sasa akiwa ameambatana na mwenzake akajibu, "Huyu hapa rafiki yangu nimemuulizia duka naye hajui." Duh jamaa akaishiwa nguvu kabisaaa.

No comments: