CHEKA TARATIBU...

Kijana mmoja akiwa kwenye mazungumzo na wazazi wake wakati wakipata chakula cha jioni, ghafla akaingia rafiki yake wa kike. Kwa kuwa baba yake alikuwa mkali sana, jamaa ikabidi apige hesabu za haraka kuzima soo. Akamfuata yule binti kwa kasi na kusema,”Vipi umefuata kile kitabu cha MBONA UMEKUJA HADI HUKU?” Yule binti  kwa akili za chap chap akaelewa somo na kujibu, “Hapana, nimefuata kitabu cha SIKUJUA KAMA WAPO.” Jamaa akaendelea, “Hicho sina ila kipo NENDA KANINGOJEE KWENYE MPERA.” Binti akajibu, “Aah hicho nimeshakisoma kwani kile cha POA USICHELEWE KUJA BASI huna? Jamaa akasema, "sina ila nataka kununua kile cha NENDA WASIJE WAKATUSHITUKIA.” Binti akajibu, “Haya jamani nakwenda, nitakuja kukichukua ukishanunua.” Baada ya binti kuondoka baba wa yule kijana akafuraaaaahi na kumpongeza kijana wake kwa kujali masomo. Duh, mjini shule jamani!

No comments: