Sunday, March 4, 2012
CHEKA TARATIBU...
Wakati akifanya mazoezi ya hesabu, mtoto mmoja mtukutu kwa bahati mbaya akajikuta akimeza ka-penseli kake wakati alipokuwa akijaribu kuiweka mdomoni ili afungue ukurasa mwingine wa kitabu. Mama yake aliyekuwa kando kwenye kochi kuona hivyo haraka akainua simu na kumpigia simu dokta wa familia. Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo; Mama: "Dokta uko wapi?" Dokta: "Nipo baa napooza koo kidogo, kuna nini?" Mama: "Mwanangu kameza penseli wakati akifanya mazoezi ya hesabu." Dokta: "Ohoo, sasa mwambie atumie peni wakati mie natafuta usafiri wa kuja huko." Mama akabaki kaduwaa. Duh, hakika ulevi noma.
This is a blog that brings you hot news that aims to educate the community about various things including sports, culture, art, entertainment and social. This blog does not involve political issues at all. We ask for your cooperation and to contribute opinions on the various information we bring to you.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment