CHEKA TARATIBU...
Dereva Taxi mmoja wa maeneo ya jirani na Las Vegas Casino, Dar es Salaam kapata abiria mwenye asili ya Japan. Wakiwa njiani yule abiria akavunja ukimya, "Hii gari inaenda taratibu mno, ungenunua gari ya Japan iko fasta sana." Yule dereva akamtazama tu yule Mjapani na kuendelea na safari. Walipofika maeneo ya Masaki yule Mjapani akamwashiria dereva kwamba ameshafika. Akashuka na kuuliza ni kiasi gani. Yule dereva akajibu, "Laki mbili tu." Mjapani akashtuka na kusema, "He, mbona nyingi hivyo?" Ndipo dereva akamjibu, "Sio mimi, ni hii mita, imetengenezwa Japan inasoma fasta sana." Duh!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment