Tuesday, March 13, 2012

BINTI WA WHITNEY AGOMA KUTUMIA JINA LA BABA YAKE

Bobbi Kristina Brown, binti wa hayati Whitney Houston ametangaza nia yake ya kubadilisha jina hilo ili kuepuka ukaribu na baba yake, Bobby Brown, imeelezwa.
Binti huyo aliwaeleza marafiki zake kwamba miaka kadhaa iliyopita alitaka kutimiza dhamira yake hiyo ya kubadili jina lakini mama yake Whitney hakumruhusu kufanya hivyo.
Kwa sasa Whitney hayupo, Bobbi mwenye miaka 19 amepania kubadilisha kabisa jina na anataka kutambulika kama Kristina Houston.
Imeelezwa kwamba Bobbi amechukua uamuzi huo akiwa katika hali ya kawaida na sehemu salama zaidi kuliko alivyokuwa siku zilizopita.
Mpaka sasa, haijafahamika lini hasa atatekeleza rasmi zoezi hilo la kubadili jina.

3 comments:

ZIRO said...

Huyu binti mbona hajatulia? Hata arobaini ya mama yake bado ashaanza mapepe! Inabidi wakubwa wamkanye..

ZIRO said...

Huyu mtoto naye mapepe. Hata arobaini ya mamake haijaisha tayari kazua mapya...

Anonymous said...

Hata arobaini bado kashaanza kuibua stori mpya. Kweli mapepe huyu binti...