Akiwa na umri wa miaka 83, Joe Jackson ambaye ni baba wa gwiji wa muziki wa Pop duniani, Hayati Michael Jackson "Wacko Jacko" juzi ametoa kali ya mwaka pale alipotinga kwenye klabu ya usiku mishale ya saa nane mjini Las Vegas, Marekani.
Baba huyo alionekana akiponda raha kwenye mgahawa wa Lavo Champagne Brunch uliopo ndani ya Hoteli ya Palazzo ambao ni maarufu kwa vyakula vya Kifaransa, akiwa katika mitoko ya ki-klabu klabu.
Vyanzo vya habari vimesema, Mzee Joe aliongozana na rafiki yake mwanaume na wakati wote alionekana akinywa maji tu. Kwenye meza aliyokaa alizingirwa na visichana na kuna wakati alitoa kamera yake na kumpa rafiki yake akimtaka apigwe picha pamoja na visichana hivyo.
Baada ya picha, wasichana walimfagilia mzee huyo kwa kumwita "Mzee Kijana" mwenye mvuto. Hivyo ndio vituko vinavyozingira jiji la Las Vegas.

No comments:
Post a Comment