Saturday, February 18, 2012
KILIO CHA WAKAZI CHANGANYIKENI
Kipande cha Barabara kati ya Majumba Ishirini, Changanyikeni kuelekea mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu eneo la Yombo kama kilivyokutwa leo asubuhi. Kipande hiki kimekuwa kero kubwa kwa wakazi wa Changanyikeni wanaotumia usafiri wa daladala kwenda mjini kutokana na kutelekezwa na wahusika. Kilio cha watumiaji wa njia hiyo ni kuwekewa lami ili waweze kupita salama hasa wakati wa mvua kutokana na uongozi wa chuo hicho kusisitiza daladala zote kutumia njia hii saa moja asubuhi hadi saa moja usiku. (Picha na ziro99blog)
This is a blog that brings you hot news that aims to educate the community about various things including sports, culture, art, entertainment and social. This blog does not involve political issues at all. We ask for your cooperation and to contribute opinions on the various information we bring to you.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment