Thursday, February 16, 2012

ARSENAL YAJIWEKA PABAYA ULAYA

Timu ya soka ya Arsenal usiku wa kuamkia leo imejiweka katika wakati mgumu baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa AC Milan kwenye Uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza, mjini Milan Italia. Katika mchezo huo wa hatua ya mtoano ya 16 Bora, mabao ya Kevin Prince Boateng (15), Robinho (38, 49) na Ibrahimovic (penalti 79) yalitosha kumfanyia Send-off ya kukumbukwa Thierry Henry anayerejea Marekani baada ya kuwa kwa mkopo Emirates. Pichani Ibrahimovic (kulia) akishangilia huku Henry akiwa haamini kinachotokea San Siro.

No comments: