Sunday, May 12, 2013

MZAHA WA LEO...

*************************
Kidogo halali ni bora 
kuliko kingi haramu!!
*************************

MFANYABIASHARA ANAYELAWITI WANAFUNZI MWANANYAMALA ATIWA MBARONI...

Kamanda Charles Kenyela.
Jeshi la  Polisi  Mkoa wa Kinondoni  linamshikilia  Ahmad  Mohamed  Sharif (38), mfanyabiashara na mkazi wa Mwananyamala Msisiri ’A’ kwa tuhuma za kuwaingilia kinyume cha maumbile wanafunzi wanne wa darasa la nne wa Shule ya Msingi Misisiri ’A’.

JICHO LA TATU...


ALIYEZINDUKA BAADA YA AJALI NA KUJIGUNDUA MJAMZITO, AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME...

Gemma akiwa amembeba mtoto wake, Ruben.
Mwanamke mmoja ambaye alizinduka baada ya kuzirai na kugundua ana ujauzito wa wiki nne amesimulia furaha yake baada ya kujifungua mtoto 'kamilifu' wa kiume.

CHEKA TARATIBU...

Rasta mmoja alienda kumtembelea ndugu yake anayeishi kwenye nyumba ya chumba kimoja maeneo ya Manzese na kugonga mlango. Sauti ikatoka kwa ndani: "We nani?"

SERIKALI SASA YAZINDUKA USINGIZINI MIKATABA YA MADINI...

Wachimbaji wakiwa kazini katika mchimbo ya madini ya Mererani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa  Sospeter Muhongo amecharuka na kuagiza Serikali kuwa na hisa katika migodi yote ya madini itakayofunguliwa kuanzia sasa.

Saturday, May 11, 2013

POLISI ALIYEUA MTOTO KWA KUMPIGA RISASI MARA ATIWA MBARONI...

Kamanda Justus Kamugisha.
Askari Polisi wa Kituo cha Tarime mkoani Mara mwenye namba D. 4662 Koplo Mathew, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za uzembe uliosababisha kifo kwa risasi cha mwanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Rebu, Deus Jacob (9).

JICHO LA TATU...


KUZOROTA AFYA YA 'PAPA' BENEDICT XVI KWAITISHA VATICAN...

Benedict XVI (kushoto) akisalimiana na Papa Francis I.
Kuzorota kwa afya ya Papa Emeritus Benedict XVI kumemfanya kubakia nusu ya umbile lake la siku za nyuma, imedaiwa jana.

CHEKA TARATIBU...

Mchungaji mmoja baada ya kuwafungisha ndoa 'mashoga' wawili, akapata wakati mgumu kutamka kwamba "Sasa ninyi ni MKE na MUME". Alishindwa kutamka hivyo kwa kuwa wote wawili ni wanaume. Baada ya kutafakari kwa dakika chache akapata ufumbuzi na kutamka: "Sasa ninyi ni MAN UNITED!!" Kasheshe...

WALIOJIFANYA MASISTA WAKAMATWA WAKISAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA...

Wanawake hao watatu waliobambwa na dawa za kulevya.
Wanawake watatu wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya kupitia uwanja wa ndege wakiwa wamevalia kama masista.

MAASKOFU WASEMA SASA IMETOSHA MAKANISA KUSHAMBULIWA...

Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi ya watu watatu waliouawa kwenye shambulio la bomu kanisani mjini Arusha Jumapili iliyopita.
Wakristo wametakiwa kutolipiza kisasi juu ya maovu yaliyofanywa na kikundi cha watu kwa kurusha bomu kanisani na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 66 kujeruhiwa.

MZAHA WA LEO...

**************************************
Ujinga usio na hasara ni bora 
kuliko elimu isiyo na faida!!
**************************************

RASIMU YA MWONGOZO UUNDAJI MABARAZA YA KATIBA YATOLEWA...

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2005.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa rasimu ya mwongozo wa uundwaji wa mabaraza ya Katiba yatakayoundwa na kuendeshwa na taasisi, asasi, vyama na makundi ili kujadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ya Katiba itakayoandaliwa na Tume.

Friday, May 10, 2013

SERIKALI YAWATOLEA MAKUCHA YAKE WACHOCHEZI WA KIDINI...

Dk Emmanuel Nchimbi.
Serikali imesema kuanzia sasa haitakuwa na kigugumizi kukabiliana na wachochezi wa chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na kukiri kuwa hali imefikia hapo kutokana na Serikali kulegalega kwa dhana ya uhuru wa kuabudu.

MZAHA WA LEO...

*****************************
Hata uwe na kasi kiasi gani, 
huwezi kukimbilia kifo!
*****************************
 

RUBANI JASIRI WA KIKE AANGUKA NA HELIKOPTA KATIKATI YA MTAA...

Vikosi vya waokoaji wakishuhudia ajali hiyo.
Rubani mmoja wa kike wa helikopta amepongezwa kama shujaa baada ya kuanguka nayo ardhini kutoka umbali wa futi 3,000 katikati ya jiji lenye pilika nyingi bila kusababisha madhara yoyote makubwa nchini Hawaii.

ATAKAYETAJA WALIORUSHA BOMU KANISANI ARUSHA KUZAWADIWA MILIONI 50/-...

IGP Said Mwema.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Inspekta Jenerali Saidi Mwema ameahidi kutoa donge nono  la Sh milioni 50 kwa atakayeweza kutoa taarifa ya kumfichua mhusika au wahusika wengine wa tukio la bomu lililotokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililopo Olasiti jijini hapa.

SHEKHE PONDA ARIDHIA KIFUNGO CHAKE CHA MWAKA MMOJA NJE...

Shekhe Issa Ponda akilakiwa na jamaa zake mara baada ya huku hiyo kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, jana.
Pamoja na kuhukumiwa kifungo, Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Shekhe Issa Ponda jana hakuonekana kusononeka na kusema kilichofikiwa na Mahakama ni haki yake.

DK. KIMEI ANG'ARA MCHAKATO WA KINARA WA BENKI AFRIKA...

Dk Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei amechaguliwa kwenye mchakato wa kumtafuta kinara wa Benki wa Afrika kwa mwaka 2013, unaoendeshwa na African Banker Awards chini ya African Development Bank Group.

CHEKA TARATIBU...

Mwanafunzi mmoja mtukutu kakutana na mwalimu wake na mambo yakawa hivi. Mwalimu: "Wewe kwanini kila siku unachelewa kufika shuleni?" Mwanafunzi: "Nakaa mbali sana". Mwalimu: "Mbali mbinguni?" Mwanafunzi: "Mbinguni kwa mbele kidogo!" Kasheshe...

MAHAKAMA YA RUFAA YAMREJESHEA UBUNGE DK DALALY KAFUMU...

Dk Dalaly Kafumu.
Mahakama ya Rufaa nchini imetengua uamuzi ya Mahakama Kuu na kumrudishia ubunge Dk Dalaly Peter Kafumu (CCM) wa Jimbo la Igunga baada ya kuridhika na hoja za upande wa mrufani kuwa Jaji aliyesikiliza shauri hilo hakuzingatia matakwa ya kisheria.

JICHO LA TATU...


UCHACHE WA MABEHEWA WAKERA ABIRIA TRENI YA UBUNGO...

Abiria wakiwa ndani ya treni hiyo.
Abiria wanaotumia usafiri wa treni  kutoka kituo cha Stesheni kwenda Ubungo Jijini Dar es Salaam, wameanza kuonja ‘machungu’ ya  usafiri huo, kutokana na idadi ya mabehewa kuwa ndogo, ikilinganishwa na abira wanaotaka kusafiri.

Thursday, May 9, 2013

MREMBO AJIDUNGA MAFUTA YA KULA USONI BAADA YA KUGOMEWA NA MADAKTARI...

KUSHOTO: Hang alivyo sasa. KULIA: Hang alivyokuwa hapo awali.
Mwathirika wa utengenezaji upya viungo amejidunga sindano ya mafuta ya kupikia kwenye uso wake baada ya madaktari kugoma kumpatia silikoni zaidi.

WABUNGE WATAKA SHERIA YA KINGA DHIDI YAO ITAZAMWE UPYA...

Sehemu ya wabunge wanaounda Bunge la Jamhuri ya Muungano wakifuatilia kikao mjini Dodoma.
Baada ya kubaini kuwa wao ndio chanzo cha uvunjifu wa amani kutokana na kauli zao bungeni, wabunge wameona haja ya kuangalia upya sheria, ikiwamo ya kinga ambayo inawapa uwezo wa kutoa kauli hizo.

WILFRED RWAKATARE AFUTIWA MASHITAKA YA UGAIDI DHIDI YAKE...

Wilfred Rwakatare na wenzake wakitoka mahakamani.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema,Wilfred Rwakatare na mwenzake Ludovick Joseph wamepata nafuu kidogo baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwafutia baadhi ya mashitaka.

MZAHA WA LEO...

****************************
Hakuna Airport ya kuku 
japo naye pia ni ndege!
****************************

MAHAKAMA YA RUFAA YAHALALISHA KUACHIWA HURU KWA ABDALLAH ZOMBE...

Abdallah Zombe akiwa mahakamani.
Mahakama ya Rufaa jana ilitupilia mbali rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa Zombe na wenzake wanane.

JICHO LA TATU...