Thursday, May 9, 2013

MFUMUKO WA BEI NCHINI WAPOROMOKA HADI ASILIMIA 9.4...

Baadhi ya masoko yanayouza vyakula vya nafaka.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema mfumuko wa bei wa Taifa kwa Aprili mwaka huu, umepungua hadi kufikia asilimia 9.4 kutoka asilimia 9.8 ya Machi mwaka huu.

Wednesday, May 8, 2013

SIR ALEX FERGUSON ABWAGA MANYANGA MANCHESTER UNITED...

Muda mfupi uliopita, Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametangaza rasmi kwamba atastaafu klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa miaka 27.

UAMUZI RUFAA YA KUACHIWA ABDALLAH ZOMBE KUTOLEWA LEO...

Abdallah Zombe.
Mahakama ya Rufaa leo inatarajia kutoa uamuzi wa rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe na wenzake wanane.

CHEKA TARATIBU...

Mke wa mtu akisoma meseji kutoka kwa mwanaume wake wa nje alijikuta akitokwa machozi baada ya buzi lake hilo kumweleza mapenzi yao yamefikia kikomo.

MABAKI YA BOMU LILILORUSHWA KANISANI ARUSHA KUCHUNGUZWA...

Mabaki ya bomu hilo lililoua watu watatu na kujeruhi zaidi ya 70.
Bomu lililorushwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti Arusha litachunguzwa kubaini aina yake na lilikotengenezwa.

JICHO LA TATU...


KESI YA WILFRED RWAKATARE KUUNGURUMA TENA LEO...

Wilfred Rwakatare akiingia mahakamani Kisutu kusikiliza kesi dhidi yake.
Uamuzi wa ombi la marejeo ya mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Rwakatare, utatolewa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

MZAHA WA LEO...

********************************
Hata uwe na kikohozi gani, 
huwezi kupasha moto juisi!
********************************

Tuesday, May 7, 2013

BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MWAKA 2013/2014...


HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHESHIMIWA DKT. EMMANUEL JOHN  NCHIMBI   (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
KWA MWAKA 2013/2014

I. UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, baada ya kuzingatia taarifa iliyowasilishwa mbele ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba kutumia  fursa hii kutoa masikitiko yangu kwa familia na wananchi kwa ujumla kutokana na vifo, ulemavu, upotevu na uharibifu wa mali na miundombinu vilivyosababishwa na ajali za barabarani, majini, kuporomoka kwa majengo na vifusi, vurugu na fujo katika mwaka mzima wa 2012. Aidha, nawapa pole ndugu na jamaa wa marehemu waliopoteza maisha yao katika matukio hayo. Namwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

3. Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru kwa dhati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Anna Margareth Abdallah, Mbunge Viti Maalum kwa kuyachambua Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Naishukuru pia Kamati hiyo kwa maelekezo na ushauri wao wenye lengo la kuboresha utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

4. Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii pia kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake aliyoitoa mapema katika mkutano huu wa Bunge ambayo imetoa mwelekeo wa kazi za Serikali kwa ujumla katika mwaka wa fedha wa 2013/2014.

5. Mheshimiwa Spika, majukumu ya msingi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, kuhifadhi na kuwarekebisha wafungwa, kutekeleza Programu ya Huduma  kwa Jamii, kudhibiti uingiaji na utokaji nchini wa raia na wageni, kutoa huduma za zimamoto na uokoaji, kuwahudumia wakimbizi waliopo nchini, na kutoa vitambulisho vya Taifa. Majukumu haya yanatekelezwa kupitia Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Huduma kwa Jamii, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Wakimbizi na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.

DEREVA WA BODABODA MBARONI KWA KUTUPA BOMU KANISANI ARUSHA...

Hali ilivyokuwa kanisani hapo juzi.
Dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, Victor Ambrose, anatuhumiwa kurusha bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya  Olasiti jijini Arusha, lililosababisha vifo vya watu wawili na wengine karibu 70 kujeruhiwa.

BOMU KANISANI LAKATISHA ZIARA YA RAIS KIKWETE KUWAIT...

Rais Jakaya Kikwete.
Mshituko uliosababishwa na ugaidi wa bomu kurushwa kwa waumini katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya  Olasiti jijini Arusha, umemlazimu Rais Jakaya Kikwete, kukatisha ziara yake nchini Kuwait, na kurejea nyumbani haraka.

JICHO LA TATU...


NAFASI ZA UONGOZI CHADEMA SASA KUTANGAZWA MAGAZETINI...

Dk Willibrod Slaa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuanzia sasa kitatumia utaratibu mpya wa kuwapata wagombea wa uongozi ndani ya chama hicho, ambapo watatangaza nafasi katika magazeti ili wanaotaka waombe.

MAHAKAMA YA RUFANI YAMREJESHEA UBUNGE HILARY AESHI...

Mheshimiwa Hilary Aeshi.
Mahakama ya Rufaa, imemrudisha bungeni na kumtangaza Hilary Aeshi kuwa mbunge halali wa Sumbawanga Mjini, baada ya kutengua hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga iliyomuondoa madarakani.

Monday, May 6, 2013

INJINI YA NDEGE YALIPUKA NA KUWAKA MOTO IKIWA NA ABIRIA 162 ANGANI...

Injini ya ndege hiyo ikiwaka moto kama ilivyonaswa pichani.
Abiria walijawa na hofu kubwa ya maisha yao baada ya injini ya ndege kulipuka moto ikiwa maelfu ya futi juu ya usawa wa bahari.

CHEKA TARATIBU...

Babu mmoja aliingia kwenye mgahawa na kuagiza uji. Wakati akianza tu kunywa, akaingia Mzungu na kuagiza soda aina ya Fanta. Baada ya kuamaliza kunywa ile soda yule Mzungu akasema: "Fantastic". Baada ya Mzungu kuondoka, babu naye alipomaliza uji wake naye akainuka na kusema: "Ujistic!" Balaa...

MASTAA JANA NA LEO...

Msanii maarufu nchini Marekani, TYRA BANKS alivyokuwa enzi za utoto wake (kushoto) na muonekano wake wa sasa (kulia).

MZAHA WA LEO...

***********************************
Hata uwe na wivu kiasi gani, 
huwezi kumwonea wivu 
marehemu kwa kutangulia kufa!
***********************************

BOMU KANISANI LAUA WATATU, LAJERUHI ZAIDI YA WAUMINI 70 ARUSHA...

Baadhi ya majeruhi wa bomu hilo wakipatiwa huduma eneo la tukio jana.
Watu karibu 70 wamejeruhiwa na watatu kufa, wakati kitu kinachodhaniwa kuwa bomu la kutupa kwa mkono, kiliporushwa kanisani na mtu asiyejulikana wakati misa ikiendelea.

JICHO LA TATU...


HATMA YA WAGOMBEA UDIWANI ARUSHA MJINI KUJULIKANA JUMATANO...

Mandhari ya mji wa Arusha.
Hatima ya wagombea wa udiwani Jimbo la Arusha Mjini, inatarajiwa kujulikana Mei 8 mwaka huu, baada ya Kamati ya Siasa ya Mkoa kutoa majina ya wagombea katika kata hizo nne.

Sunday, May 5, 2013

BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MWAKA 2013/2014...


HOTUBA YA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MHESHIMIWA SHAMSI VUAI NAHODHA (MB.) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA  MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2013/2014

UTANGULIZI


1.         Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

2.         Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwasilisha hotuba yangu ya bajeti kwa mwaka 2013/2014 mbele ya Bunge lako Tukufu.  Pili, nawashukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu na Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais kwa kuendelea kuniamini kuiongoza Wizara ya  Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.  Namshukuru pia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda kwa maelekezo anayonipatia katika kutekeleza majukumu ya Wizara yangu. Nawathibitishia Waheshimiwa Wabunge wenzangu na wananchi kwa ujumla kwamba nitaendelea kutekeleza majukumu niliyokabidhiwa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

3.         Mheshimiwa Spika, vile vile napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ulinzi na Usalama, Mhe.  Anna Margareth Abdallah (Mb.) na Makamu Mwenyekiti, Mhe. Mohammed Seif Khatib (Mb.) kwa kuchaguliwa kuiongoza Kamati hiyo. Halikadhalika, nawapongeza Waheshimiwa Wabunge wote walioteuliwa kuwa wajumbe wa Kamati hiyo.  Ninawaomba wajumbe hao wapokee shukurani zangu kwa maoni waliyotupatia wakati wa kuchambua mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka 2013/2014. Maoni na mapendekezo yao yametusaidia sana katika kuiandaa hotuba hii.

4.         Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 28 Machi, 2013 Mbunge mwenzetu Salim Hemed Khamis, Mbunge wa Jimbo la Chambani  alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Ninaungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa pole kwako Mheshimiwa Spika, familia, ndugu na marafiki kwa msiba huo.  Namuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Peponi. Amina.

MASTAA JANA NA LEO...

Msanii maarufu The Game alivyokuwa utotoni (kushoto) na jinsi anavyoonekana sasa baada ya kuwa staa (kulia).

WAASI RDC WAONYWA WAKITIA MGUU TANZANIA WATAKIONA CHAMOTO...

Baadhi ya askari wa kundi la waasi la M23 wakirandaranda nchini DRC.
Waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanaojiita M23 wameonywa wasithubutu kuingia nchini kishari kwani wakifanya hivyo cha moto watakiona.
Lakini wanapaswa pia kujua kwamba kamwe Tanzania haitatishwa na kauli zao kwani nchi iko imara dhidi ya adui yeyote.

JICHO LA TATU...


MBAKAJI WATOTO SHINYANGA APANDISHWA KIZIMBANI...

Mtuhumiwa wa kesi ya ubakaji wa watoto,  Jacob Mayani (28), juzi alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga kusomewa mashitaka mawili ya kutenda vitendo vyenye nia ya kusababisha madhara, kubaka na kulawiti watoto wenye umri wa kati ya miaka minane na kumi, wanafunzi wa shule za msingi.

PRECISIONAIR YAWAHAKIKISHIA ABIRIA SAFARI ZA ZANZIBAR...

Moja ya ndege za Precisionair.
Uongozi wa Shirika la Ndege la Precisionair (PW), umewahakikishia wateja wake kuwa inaendelea na safari zake visiwani Zanzibar kama kawaida.

MZAHA WA LEO...

*********************************
Dobi naye anapiga pasi vizuri, lakini hawezi kupata namba timu ya Barcelona!
*********************************

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 YAANZA KUPITIWA UPYA...

Wanafunzi wakifanya mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana.
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limeanza kazi ya kupanga upya daraja la ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza mwaka jana na ambao matokeo yao yamefutwa.

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja katika kujifagilia kwa demu akajitambulisha kuwa anasomea kozi ya HOTEL MANAGEMENT. Baada ya siku kadhaa yule binti akamkuta jamaa akiosha vyombo kwa mama ntilie mmoja uswahilini na kumuuliza: "Bebi vipi, mbona uko hapa?" Jamaa kuzima soo akajitetea: "Niko FIELD!" Duh...