Sunday, May 5, 2013

MBATIA ATAKA WAZIRI KAWAMBWA AKAMATWE NA KUSHITAKIWA...

James Mbatia.
Baada ya Serikali kutoa kauli kuhusu mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka jana, Mbunge James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ametaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, awajibike na ikiwezekana akamatwe na kushitakiwa.

Saturday, May 4, 2013

HOTUBA KAMILI YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MWAKA 2013/2014....


HOTUBA YA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, MHESHIMIWA MATHIAS M. CHIKAWE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI 
YA FEDHA KWA MWAKA 2013/2014

Mathias Chikawe.
UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa yangu niliyoiwasilisha kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala tulipokutana kwa lengo la kujadili na hatimaye kupitisha maombi ya Mpango na Bajeti ya Wizara yangu, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Wizara Katiba na Sheria, uliopitishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kwa Mwaka wa fedha 2013/2014.

MASTAA JANA NA LEO...

Kweli siku hazigandi. Huyu ndiye msanii Amber Rose unajemfahamu akiwa katika picha yake ya utotoni (kushoto) na alivyo sasa (kulia).

MATOKEO MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2012 YAFUTWA RASMI...

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kigurunyembe, mkoani Morogoro wakifanya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana.
Wahitimu wa kidato cha nne mwaka jana huenda wakajikuta katika hali tofauti za ama furaha au huzuni kutokana na uamuzi wa Serikali wa kufuta matokeo ya mitihani yao na kuandaliwa upya kwa utaratibu uliotumika mwaka juzi.

JICHO LA TATU...


MZAHA WA LEO...

**************************************
Hata kama itasomwa kwa ufasaha 
na kuvutia kiasi gani, historia ya marehemu haipigiwi makofi!!
**************************************

HAYA NDIO MAJINA YA WAKURUGENZI WAPYA WA MIJI NA MAJIJI...

Hawa Ghasia.
Majiji manne nchini yamepata wakurugenzi wapya baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za Arusha, Mwanza, Dar  es Salaam na Mbeya.

CHEKA TARATIBU...

Panya alikuwa kapiga magoti anasali kanisani. Mara alipotazama pembeni akamwona paka amekaa. Panya akasema kwa woga: "Hapa tuko kanisani bwana, habari zako za kukimbizana na kulana hazitakiwi hapa!" Paka akajibu: "Hapa tunakula hadi mwili wa Yesu, sembuse wewe? Hebu maliza kusali nakusubiri kwa hamu!!" Kasheshe...

SERIKALI YAPANGA KUANZISHA MAHAKAMA ZA KESI NDOGO...

Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe.
Serikali ina mpango wa kuanzisha mahakama ndogo zitakazoshughulikia kesi ndogo pekee kama vile matatizo ya Wamachinga na wizi mdogo, ili kutoa fursa kwa mahakama nyingi kushughulikia kesi kubwa na kupunguza mlundikano wa kesi.

Friday, May 3, 2013

MASTAA JANA NA LEO...

Mwimbaji maarufu nchini Marekani, Kelly Rowland alivyokuwa enzi wa utoto wake (kushoto) na alivyo sasa (kulia).

NDEGE ZA PRECISION AIR ZAPIGWA 'STOP' KURUKA AU KUTUA ZANZIBAR...

Moja ya ndege za Precision Air ikiwa angani katika moja ya safari zake.
Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB), imetoa amri ya kuzuia kutua na kuruka kwa ndege za kampuni ya Precision Air Service Co. Ltd, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, kutokana na kutolipa zaidi ya Sh bilioni 37.2 zinazotokana na malimbikizo ya malipo ya ada ya huduma ya uwanja wa ndege.

JICHO LA TATU...


SHULE BINAFSI ZATAKIWA KUREKEBISHA ADA ZAO...

Moja ya shule binafsi nchini, Mairiva Secondary School iliyoko mkoani Arisha.
Shule zinazoendeshwa na kumilikiwa na taasisi na watu binafsi, zimetakiwa kurekebisha ada zao ili Serikali iangalie uwezekano wa kushirikiana nazo katika kulipia.

MZAHA WA LEO...

**************************************
Hata uwe Mkurugenzi wa Bandari, 
huwezi kurudi  kwako na meli!
**************************************

CHEKA TARATIBU...

Jamaa kaenda kutoa posa kwa binti fulani. Wazazi wakamkatalia kwa sababu binti yao bado yupo shuleni anasoma. Jamaa baada ya kufikiri kwa muda akajibu: "Haina shida wazee, basi nitakuja wakati wa mapumziko!" Duh, kasheshe...

HUKUMU YA SHEKHE PONDA SASA KUTOLEWA ALHAMISI IJAYO...

Shekhe Ponda Issa Ponda.
Kesi ya uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya Sh milioni 59, inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekhe Issa Ponda na wafuasi wake 49, jana ilitajwa  kwa mara ya mwisho kabla ya kutolewa hukumu wiki ijayo.

Thursday, May 2, 2013

RAPA CHRIS KELLY WA KUNDI LA KRISS KROSS AFARIKI DUNIA


Chris Kelly, mmoja wa wasanii wawili wa kundi la Kriss Kross lililotamba katika miaka ya 1990 ambao walidumu kwa miaka 10 ya nyimbo za kukumbukwa kikiwamo kibao cha "Jump", amefariki dunia mapema leo kwenye hospitali moja mjini Atlanta kwa kile kinachodaiwa kujizidishia dozi ya dawa nyumbani kwake, imeelezwa. Alikuwa na umri wa miaka 34.
"Inaonesha kuna uwezekano wa kuzidisha dozi ya dawa," alisema Koplo Kay Lester, msemaji wa Polisi wa Fulton County.
Hii, alisema Lester, inatokana na taarifa zilizopokelewa kwenye eneo la tukio na pia ushahidi uliopatikana nyumbani kwa Kelly huko kusini Atlanta.
Kwa mujibu wa Lester, polisi waliitwa nyumbani kwa Kelly majira ya mchana. Alipelekwa kwenda Kituo cha Afya cha Atlanta.
Mchunguzi Betty Heney wa Ofisi ya uchunguzi ya Fulton County alisema Kelly alitangazwa kufa katika hospitali hiyo mapema leo.
Hakuna sababu rasmi za kifo chake zilizoelezwa, kusubiria uchunguzi.
Kelly, aliyefahamika kama "Mac Daddy," na Chris Smith, alifahamika kama "Daddy Mac," walivumbuliwa kwenye ulimwengu wa muziki mwaka 1992 na prodyuza wa muziki na rapa Jermaine Dupri baada ya kuwagundua wawili hao kwenye ukumbi mmoja mjini Atlanta. Wawili hao walikuwa wakivaa nguo zao kinyume, lakini waliweza kuwateka mashabiki kwa rapu zao.
Wimbo wao wa kwanza uliowapatia mafanikio makubwa ulikuwa "Jump." Kibao hicho kilikuwa kwenye albamu yao iliyofanya vizuri sana mwaka 1992 ya "Totally Krossed Out."
Wawili hao walishangaza mashabiki kwa ukomavu wao katika rapu, ingawa wimbo huo uliandikwa na Dupri.

MASTAA JANA NA LEO...

Mwanamuziki maarufu duniani, Justin Bieber alivyokuwa utotoni (kushoto) na muonekano wake wa sasa (kulia).

MZAHA WA LEO...

******************************
Ugali hata uwe na moto kiasi gani, 
lakini hauwezi kuwashia sigara!
******************************

SERIKALI YATANGAZA KUPUNGUZA KODI KATIKA MISHAHARA...

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akishikana mikono na viongozi wengine kuimba wimbo wa Mshikamano Daima wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya jana.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Philemon Mgaya, mke wa Rais Mama Salma,Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, Kaimu Rais wa TUCTA, Nortubunga Maskini, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na Katibu Mkuu wa CCM  Abdulrahman Kinana.
Wafanyakazi nchini watapata nafuu kimapato, pale Serikali itakapoanza kutekeleza azma yake ya kupunguza kodi kwenye mishahara (PAYE) wiki mbili zijazo.

NDEGE YA ABIRIA YANUSURIKA KUGONGA KITU KINACHOELEA ANGANI...

Ndege ya abiria ilifikia hadi ukaribu wa ndani ya futi 300 za kugongana na kitu ambacho hakikutambulika kilichokuwa kikielea angani, wachunguzi rasmi wameelezwa.

WABUNGE WATWANGANA MAKONDE NDANI BUNGENI...

Bunge la Venezuela.
Makonde yameibuka bungeni na baadhi ya wabunge kujeruhiwa katika sintofahamu, kutokana na mjadala kuhusu uchaguzi wa hivi karibuni unaobishaniwa.

BABU ACHOMWA VISU NA KUFA AKITOKA SALA YA JIONI MSIKITINI...

KUSHOTO: Sehemu yalipotokea mauaji hayo. KULIA: Muhammed Saleem Chaudhry.
Babu amechomwa visu na kufa hatua chache kutoka mlango wa nyumba yake wakati akirejea nyumbani hapo kutoka kwenye sala ya jioni msikitini.

KAMPUNI WW ZA KITALII KUFUTWA HIFADHI YA RUAHA...

Mandhari ya Hifadhi ya Ruaha.
Shirika la Hifadhi Tanzania (TANAPA) limepewa miezi sita, liwe limefuta kampuni 11 zilizopewa maeneo ya kujenga ndani ya hifadhi ya Ruaha tangu Juni mwaka 2009 na kushindwa kufanya ujenzi. 

JICHO LA TATU...


MZEE ALFRED TANDAU AFARIKI DUNIA, JK ATUMA RAMBIRAMBI...

Rais Jakaya Kikwete ameelezea kushtushwa na taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwekahazina wa  Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alfred Tandau.
Mzee Tandau, ambaye ni kiongozi wa miaka mingi wa wafanyakazi na Waziri wa muda mrefu wa Serikali,   aliaga dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) mjini Dar es Salaam, ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu ya saratani ya tumbo.
Katika salamu zake kwa Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema amepokea kwa mshituko na masikitiko taarifa za kifo cha Mzee Tandau.
“Nakutumia wewe Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Kinana salamu zangu za dhati za rambirambi kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako nawatumia rambirambi viongozi na wanachama wote wa CCM kwa kumpoteza kiongozi na mwanachama mwenzetu.
“Aidha, kupitia kwako, naomba ufikishe salamu nyingi za pole kwa familia kwa kuondokewa na kiongozi na mhimili wa familia. Wajulishe kuwa niko nao katika kuomboleza kifo cha kaka yetu na kiongozi mwenzetu na naelewa machungu yao katika kipindi hiki. Napenda wajue kuwa naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya marehemu. Amina,” alisema Rais Kikwete.
Alisema alimfahamu Alfred Tandau kwa miaka mingi. Alikuwa kiongozi hodari na mwaminifu ambaye katika nafasi zote alizozishikilia katika utumishi wake wa umma, alithibitisha uadilifu na uzalendo wa kiwango cha juu.
“Katika uongozi wa Chama cha Wafanyakazi (NUTA) na baadaye Juwata, Mzee Tandau alijipambanua kuwa mtetezi halisi na mkweli wa maslahi ya wafanyakazi. Katika Serikali ambako alitumika miaka mingi kama Waziri, alikuwa mwaminifu na mtii kwa Serikali yake, kwa viongozi wake na kwa wananchi aliowatumikia,”   alisema Rais Kikwete.
Alisema katika nafasi yake ya Mwekahazina wa CCM,  aliendeleza sifa hizo hizo alizokuwa nazo tangu awali. “Tutakosa sana busara na ushauri wake.”

Wednesday, May 1, 2013

ADAIWA KUNAJISI WATOTO KISHA KUWATOBOA MACHO...


Evarist Mangala.

Mtuhumiwa sugu wa matukio ya unajisi na vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, anashikiliwa Polisi mkoani Shinyanga, baada ya kukurupushwa katika jaribio la kutaka kumnajisi na kumtoboa macho mwanafunzi mwenye umri wa miaka minane.

MEMBE AOTESHWA KUGOMBEA URAIS UCHAGUZI MKUU 2015...


Bernard Membe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015, iwapo wananchi wataona anafaa na kumtaka afanye hivyo.

JICHO LA TATU...


IDDI SIMBA SASA ASHITAKIWA KWA KUHUJUMU UCHUMI...


Iddi Simba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Iddi Simba aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka ya kusababisha hasara katika shirika hilo, amefutiwa mashitaka hayo na kusomewa mapya ya uhujumu uchumi.