Friday, May 9, 2025

'FATHER NKWERA' WA MAOMBEZI YA BIKIRA MARIA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Padri wa Kanisa Katoliki, Felician Nkwera aliyejizolea umaarufu kwa kufanya maombezi ya Bikira Maria, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.Nkwera ambaye kituo chake cha maombezi cha Bikira Maria kipo Ubungo Riverside, Dar es Salaam amefariki dunia leo Ijumaa akiwa Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam, kwa matatizo ya baada ya shinikizo la damu.
Mwenyekiti wa kituo hicho, Deogratias Karulama alithibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema, Padri Nkwera alipata tatizo la kushuka kwa shinikizo la damu na kukimbizwa hospitali na baada ya kurudia vipimo vilionesha hana tatizo lolote.
“Walimwekea dripu lakini baadaye shinikizo
la damu likashuka tena, aliwaambia waumini ambao walimpeleka kwamba msiogope, akafunga macho yake,” alieleza.
Alisisitiza: “Kimsingi wakati wanatangaza tunaye, Papa majira ya saa 5:51 asubuhi kwa saa za Ulaya, Tanzania ikiwa saa 2:00 usiku, yeye alifunga macho yake na kuaga dunia.”
Aliongeza: “Tutatoa taarifa kuhusu siku ambayo kiongozi wetu atazikwa, tu-nategemea waumini kutoka Poland, Norway, Kenya, Uganda na mataifa mengine waje kushiriki nasi kum-pumzisha baba yetu”. Padri Nkwera aliza-liwa Luilo katika Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe, Aprili 28, 1936. Wazazi wake ni Venant Nkwera na Em-maculata Mhagama.
Alitengwa na Kanisa Katoliki kutokana na kukosa utii kutoka kwa viongozi wake.
Pia, alikuwa mwandishi wa vitabu Tumbuizo la jioni (1968), Johari Ndogo (1979), Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo (1979), Kiswahili Sekondari na Vyuo (1979), Maana na Lengo la Adhabu ya Kifungo (1987) na Tamrin za Fasihi Simulizi, Sekondari na Vyuo (1998).
Nkwera alipata Daraja Takatifu la Upadri mwaka 1968 na kuanza huduma ya maombezi akiwa bado padri kijana mkoani Tabora na baa-daye kuhamia Dar es Salaam.
Alitoa huduma hiyo ambayo ilimfanya aingie kwenye mgogoro mkubwa na jimbo alilokuwa akili-hudumia wakati huo hata kufikishwa makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na baadaye Roma.
Inaelezwa wenye imani kuhusu maombezi yake, wamekuwa wakikiri kwa kinywa na maandishi kwamba wameponywa huku rozari, maji ya baraka na sala vikiwa ndiyo msingi mkuu wa maombi yake.
Baadhi ya watu walikosoa huduma zake wakihusisha na ukosefu wa utii kwa aliyekuwa kiongozi wake kwa wakati huo alipokuwa Jimbo Katoliki la Njombe na pia, hakutii maamuzi na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wake wakubwa yaani maaskofu, TEC na hata Kadinali Polycarp Pengo kwa wakati huo.

No comments: