Daraja
jipya la Kigamboni ambalo sasa litajulikana kama "Daraja la Nyerere" lililozinduliwa rasmi jana na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, kama
linavyoonekana pichani. Daraja hili ndilo kubwa na la kisasa zaidi
katika ukanda huu wa Afrika Mashariki likiwa na urefu wa mita 680.
Daraja hili lina barabara sita za kupita magari, tatu kila upande. Pia
lina njia za waenda kwa miguu zenye upana wa mita 2.5 moja kila upande.
Kuna taarifa zilizozagaa zenye kupotosha kwamba eti daraja hili liko
katika nchi jirani ya Kenya. Ni uongo... Daraja hili lililobatizwa jina
ya DARAJA LA NYERERE liko jijini Dar es Salaam katika wilaya mpya ya
Kigamboni. |
No comments:
Post a Comment