Mfanyakazi
wa ndani, Joseph Matonya (26) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko
12 baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mwanafunzi wa kidato cha pili katika
shule ya sekondari Mwanagati mwenye umri wa miaka 14.
Akisoma
hukumu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hakimu John Msafiri alisema
kuwa mshitakiwa huyo atatumikia adhabu ya viboko ambavyo atachapwa sita
akiingia na sita akitoka.
Pia
alisema Matonya atatakiwa kulipa fidia ya Sh milioni moja baada ya kumaliza
kifungo hicho.
Hakimu
Msafiri alisema mshtakiwa alitiwa hatiani baada ya upande wa mashitaka
kuthibitisha mashitaka yake bila ya kuacha shaka kwa kuwa na mashahidi wanne na
PF3 iliyothibitisha kubakwa kwa mwanafunzi huyo.
Hata
hivyo, Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda alidai kwamba mshtakiwa apewe adhabu
kali iwe fundisho kwa wengine.
Kabla
ya hukumu, mshitakiwa huyo alidai kuwa
yeye ni mgeni wa Mahakama na kwamba familia yake inamtegemea na kudai kuwa
hakumbaka mtoto huyo.
Pia
alidai kuwa adhabu hiyo imemuathiri kisaikolojia na kimwili na kwamba hatasahau
maishani mwake.
Ilidaiwa kati ya Novemba na Desemba,
2013, maeneo ya Kitunda Mwanagati, wilayani Ilala, Matonya alimbaka mtoto wa
miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari
Mwanagati.

No comments:
Post a Comment