Serikali imeelezea
kusikitishwa na uamuzi wa Kenya wa kuzuia magari ya kitalii ya Tanzania kwenda
kuchukua na kushusha watalii wanaotumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta, kwa kusema kuwa hatua hiyo haijengi wala kuendana na dhamira njema ya
mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Waziri wa Afrika
Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe alisema jana kuwa, dhamira ya kuanzishwa
upya kwa jumuiya hiyo haiendani na tukio la aina hiyo.
Hata hivyo alisema kwamba
Serikali ya Tanzania itaendelea kuheshimu na kuzingatia amri
iliyotolewa na Kenya ili kulinda undugu na urafiki uliopo kati ya nchi
hizo huku
wakitafakari hatua za kuchukua kuondoa bughudha iliyotokea kwa watalii
na wasafiri wanaopitia uwanja huo.
wakitafakari hatua za kuchukua kuondoa bughudha iliyotokea kwa watalii
na wasafiri wanaopitia uwanja huo.
Waziri Mwakyembe alieleza
kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea na mchakato ulioanzishwa wa kuhusisha
wadau wote wanaoguswa na tatizo hilo hadi kufikia uamuzi ambao
utauwasilisha kwa Serikali ya Kenya kupitia vikao rasmi vya Jumuiya.
Hata hivyo, alisema
pamoja na kwamba amri hiyo ya Serikali ya Kenya inakwenda nje ya mkataba wa
1985 kwa kuvihusisha hata viwanja vya ndege kuwa sehemu ya vivutio vya utalii,
Serikali ya Tanzania itaheshimu na kuzingatia amri hiyo ili kulinda undugu na
urafiki uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Alisema pia kwamba
Serikali itatafakari hatua za kuchukua ili kuondoa bughudha kubwa itakayotokea
kwa watalii na wasafiri wanaokuja nchini wanaopitia uwanja huo wa Jomo
Kenyatta.
Alizitaja hatua hizo kuwa
ni pamoja na kuwafahamisha watalii na wageni wote wenye nia ya kutembelea
vivutio vya kitalii vya Tanzania kutumia viwanja vingine vya ndege ili kuepuka
kadhia na gharama zisizo za lazima.
Waziri huyo alisisitiza
kuwa viwanja vya ndege hasa vile vya kimataifa vitaendelea kuwa sehemu ya
milango ya kuingilia na kutokea kwenda kokote ndani ya Jumuiya au nje ya
Jumuiya na havitachukuliwa kama vivutio vya utalii.
"Tanzania haitazuia
magari ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au nchi nyingine yoyote
kuingia katika viwanja vyake vya ndege kuleta au kuchukua watalii wanaopitia
katika viwanja hivyo na kwenda katika nchi zao," alisema.
Dk Mwakyembe ambaye ni
Waziri mpya kwenye wizara hiyo alisema mkataba wa mwaka 1985 kati ya Tanzania
na Kenya ulilenga kutoa mwongozo wa ushirikiano katika Sekta ya Utalii kati ya
nchi hizo mbili.
Aliongeza kuwa
makubaliano hayo yalielekeza maeneo muafaka kwa ajili ya kubadilishana watalii
huku ikizingatiwa kuondoa bughudha kwa watalii.
Maeneo hayo ni pamoja na
miji ya mipakani na miji rasmi iliyopendekezwa na kukubalika na pande zote
mbili ikiwemo Nairobi ambako Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta
kipo.

No comments:
Post a Comment