Chama cha Wananchi (CUF) mjini Lindi kimepata
wanachama wapya kutoka CCM wapatao 891 kuanzia mwezi Desemba mwaka jana hadi
Februari mwaka huu.
Katibu wa chama hicho mjini hapa, Rashidi
Ndauka alisema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili ofiisni
kwake mjini hapa.
Alisema wanachama hao wamegawanyika sehemu kuu
mbili, ambako wanachama 775 ni wanachama wapya na 116 wanatokea CCM wakiwemo na viongozi wao.
Ndauka alisema viongozi waliojiunga na chama
hicho na Mwenyekiti wa CCM kata ya Ngapa, Hamisi Nganga kutoka tawi la Mkwaya,
ambako katibu wa tawi hilo, Abdallah Mchewa alijiunga na chama hicho.
Katibu huyo wa CUF alisema tatizo
lililowafanya wanachama hao wa CCM wakihame chama chao na kujiunga na CUF ni
kutokana na huduma ya maji waliyoipata ambayo imetokana na juhudi binafsi za
mbunge wa jimbo la Lindi Mjini, Salumu Baruany.
Alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa
wananchi hao kupatiwa huduma ya maji licha ya kuwa miaka ya nyuma jimbo hilo
lilikuwa linaongozwa na CCM.
Pia, alisema wananchi wa jimbo hilo walikuwa
na matatizo mengi, ikiwemo ukosefu wa mbegu bora za mazao, hali inayofanya
wakulima wanakuwa na wakati mgumu katika upatikanaji wa pembejeo hizo, kwa
ajili ya kuzitumia mashambani, mwaka kipindi cha kilimo.
Mwenyekiti wa CUF na Mbunge wa Lindi Mjini
kupitia CUF, Salumu Baruany aliwashauri wananchi wajiunge na chama hicho, kwani
itakuwa rahisi kwao kupata maendeleo yao.
Alisema kwamba kipindi kifupi chama chake
kimejitahidi kuibana Serikali kujenga barabara za mjini, mradi wa maji wa
Ng’apa na kuboresha miundombinu mbalimbali.
Baruany alisema kama wananchi wataamua
kujiunga na upinzani, basi watakuwa wanapata maendeleo, kwani mikoa ya
Kaskazini ambako wapinzani wapo wengi na kuna maendeleo mazuri, miundombinu ya
kielimu, nishati za umeme, majengo ya shule na zahanati ni bora.

No comments:
Post a Comment