Meneja wa
kituo cha mafuta cha Gudal Petrol Station cha Ubungo, Kibangu pamoja na
mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamepandishwa kizimbani kwa
mashitaka mawili likiwamo la wizi.
Watuhumiwa
hao, Meneja Saadi Mohamed (21) na mwanafunzi Edwin Mbuya (21), wote wakazi wa
Ubungo-Kibangu, walipandishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni
wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la wizi wa fedha taslimu Sh milioni
51.6 mali ya kituo hicho.
Mbele ya
Hakimu Kwey Rusema, Wakili wa Serikali, Credo Rugaju, alidai kuwa katika
shitaka la kwanza, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa katika tarehe
na muda usiyojulikana maeneo ya Kinondoni.
Katika
shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Julai 28 mwaka huu, washtakiwa waliiba fedha
taslimu Sh 51,689,500, mali ya Kituo cha Gudal Petrol Station kilichopo Ubungo
Kibangu. Washtakiwa walikana na upelelezi umekamilika. Kesi imepangwa
kusikilizwa Agosti 19 mwaka huu.
Katika
hatua nyingine, mkazi wa Mbezi Luis, Omary Kupaza (32), amefikishwa katika
Mahakama hiyo akikabiliwa na kosa la kumbaka mtoto wa miaka 14.
Mbele ya
Hakimu Izhaq Kuppa, wakili wa Serikali, Masin Mussa, alidai kuwa tukio hilo ni
la Desemba 2013 huko eneo la Mbezi Msigwa ambapo mshtakiwa alimbaka mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali
sehemu za siri.
Mshtakiwa
alikana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo unaendelea. Mshitakiwa
alirudishwa rumande kwa kushindwa masharti ya dhamana na kesi hiyo imepangwa
Agosti 19.
No comments:
Post a Comment