Zaidi ya asilimia 23 ya wanawake wenye umri wa kuzaa, wamegundulika kuwa na uzito uliokithiri ambao pamoja na athari za kiafya, kwa upande wa wajawazito unahatarisha afya kwa mtoto anayezaliwa.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Florens Turuka
alisema hayo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu inayohusisha wataalamu
kutoka Umoja wa Mataifa (UN), sekta binafsi na wadau mbalimbali wa masuala ya
lishe nchini.
Kwa mujibu wa Dk Turuka, uzito uliokithiri kwa
wanawake licha ya kuwaweka katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo, wakati
mwingine inaweza kusababisha kuzaliwa kwa watoto wenye uzito mdogo.
Hali hiyo ya uzito uliokithiri, imetajwa kusababishwa
na matumizi ya vyakula vyenye protini kwa wingi bila ya kufanya mazoezi pamoja
na mifumo ya maisha waliyojiwekea wanawake.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Profesa
Joyce Kinabo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), alisema
matumizi ya vyombo vya usafiri hususani magari ni miongoni mwa mambo
yanayochangia uzito uliokithiri.
“Unakuta wanawake wakitoka nyumbani wanapanda kwenye
magari yao hadi ofisini, wakishamaliza kazi zao wanapanda magari kurudi
nyumbani bila kufanya mazoezi mengine,” alisema Profesa Kinabo.
Katika hatua nyingine,
semina hiyo ilielezwa asilimia 53 ya wanawake wenye ujauzito wana
matatizo ya upungufu wa damu kutokana na lishe duni.
Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Charles Pallangyo aliwaasa wanawake wajawazito kuzingatia lishe bora
kuhakikisha watoto wanaozaliwa wanakuwa na afya bora.
No comments:
Post a Comment