Wednesday, July 16, 2014

WAFANYABIASHARA WATEGEWA MAWE MAKUBWA BARABARANI NA KUPORWA

Wafanyabiashara 30 wameporwa fedha taslimu na  vitu vyao  vya   thamani vinavyokadiriwa  kwa pamoja kuwa  na thamani ya zaidi ya Sh milioni 20 wakati lori walilokuwa wakisafiria lilipovamiwa na majambazi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Frednand Rwegasira alithibitisha kutokea kwa tukio hilo  Julai  14 , mwaka huu,  saa mbili usiku  kwenye kona  za Mlima Muze  wilayani Sumbawawanga  katika barabara  ya Ntendo – Muze.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda huyo, wafanyabiashara  hao  walikuwa  wakitokea mnadani  kijijini Muze  na walikuwa  wakirejea  mjini Sumbawanga wakitumia gari  lenye namba za usajili T 714 BGZ lililokuwa likiendeshwa na Salum Said (36) mkazi  wa eneo la Mazwi  mjini hapa.
Akisimulia mkasa huo, Rwegasira alibainisha kuwa  gari hilo  aina ya Fuso  likiwa na  wafanyabiashara 30 lilipofika  katika kona kali  za Mlima Muze  walikutana na majambazi  sita  wakiwa  na mapanga, rungu  na bunduki   na kuziba barabara kwa mawe makubwa.
Baada ya  kufyatua  risasi hewani  waliwalazimisha wafanyabiashara hao kusalimisha  vitu vyao  vya thamani  zikiwemo simu za mkononi na  fedha  taslimu .
Alithibitisha kuwa  hakuna mtu  yeyote aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha katika mkasa  huo.

No comments: