Uzalishaji umeme katika kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) umefikia megawati 100, ambacho ni kiwango cha juu cha uwezo wa mitambo yake.
Kiwango hicho kilifikiwa Juni 15 mwaka huu, huku uongozi wa kampuni hiyo ukiahidi kutekeleza mipango mkakati yake yote ya utanuzi kwa awamu.
Hayo yalibainishwa na Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/Pan African Power Solutions (PAP), Joseph Makandege alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alikuwa akizungumzia maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za viongozi wa kampuni hiyo kwa umma na mamlaka za serikali tangu PAP iliponunua IPTL.
“Juni 15, mwaka huu, mitambo ya IPTL iliyopo eneo la Tegeta, ilianza kuzalisha megawati 100 za umeme, ambazo ndiyo uwezo wa mitambo hiyo. Hii ni moja ya ahadi zilizotolewa na uongozi wa PAP wakati wa ununuzi wa mitambo ya IPTL,” alisema Makandege.
Alisema IPTL ambayo inamilikiwa na kampuni ya kizalendo ya Pan African Power Solutions Tanzania Limited, inaendelea na jitihada zake za kutimiza ahadi yake ya kupunguzia wateja adha ya gharama ya umeme Tanzania.
“Tumepanga kuzalisha megawati 200 kwa kutumia mitambo inayoendeshwa kwa kutumia gesi ifikapo Desemba mwaka 2015, ambapo tutauza umeme wake kwa chini ya dola nane za kimarekani, ikiwa ni awamu ya kwanza ya utanuzi. Katika awamu ya pili ya utanuzi, tumepanga kuzalisha megawati 300 ifikapo Desemba mwaka 2017.
“Tuliahidi kupunguza bei zetu, kuongeza uzalishaji mpaka kufikia kiwango cha juu cha mitambo yetu na kuendelea kutanua mitambo yetu ili kuweza kuzalisha megawati 500 baada ya kibadilisha mfumo yake iweze kutumia gesi,” alisema.
Alisisitiza, “Hatua hii itawezesha IPTL kupunguza zaidi bei zake hadi kufikia kati ya senti sita na nane za kimarekani kwa kila uniti. Ndani ya kipindi hiki kifupi, tumeweza kudhihirisha uwezo wetu wa kutimiza ahadi zetu zote.”
Alisema bei ya umeme kwa kampuni yao kwa sasa ni kati ya senti 26 na 30 za Marekani kwa uniti. Lakini, alisema hivi karibuni bei itapungua baada ya kampuni kubadilisha mashine zake na kuanza kutumia gesi kuzalishia umeme.
Makandege aliongeza kuwa mitambo yote ya IPTL, imefanyiwa marekebisho makubwa baada ya kufanya kazi kwa zaidi ya miaka sita bila matengenezo.
Alisema uongozi mpya, unaendelea na uboreshaji wa barabara zote za ndani ya kiwanda kwa kiwango cha lami, pamoja na marekebisho mengine ambayo yatabadilisha muonekano mzima wa IPTL.

No comments:
Post a Comment