Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imeendelea kuhadharisha juu ya upepo mkali unaoambatana na mawimbi makubwa katika maeneo yote ya ukanda wa Pwani ulioanza jana.
Upepo huo unaotarajiwa kuendelea hadi kesho na maeneo ambayo TMA ilisema yamekumbwa ni Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam,Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba kwa kiwango cha asilimia 80.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka hiyo inasema hali ya upepo mkali unaozidi kilometa 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa yanayozidi meta 2.0 inatarajiwa katika ukanda wote huo, kuanzia Julai 9 hadi 12 mwaka huu.
Ilisema hali hiyo inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika maeneo ya kusini mwa Afrika hivyo kusababisha upepo mkali wa kusini, mashariki mwa Pwani ya Tanzania.

No comments:
Post a Comment