Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL) imeingia makubaliano ya kuuziana umeme na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa kiwango cha MVA 40 katika kituo chake cha Pongwe mjini Tanga.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini jijini Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Decklan Mhaiki alisema mkataba huo unalenga kuboresha ufanisi wa kazi kati ya mashirika hayo mawili na kuboresha hali ya uzalishaji.
"Kampuni ya Saruji ya Tangai ni wateja wetu wakubwa na wa muda mrefu kwa kuzingatia hayo tumekubaliana kuwauzia umeme kupitia kituo chao cha kuzalisha umeme katika mji wa Pongwe katika hatua itakayoongeza ufanisi wao wa kazi,” alisema.
Alisema makubaliano hayo yataiwezesha Tanesco kuzalisha karibu MVA 40 na kuwauzia Kampuni ya Saruji ya Tanga ambao kwa sasa wanapata MVA 20 kupitia kituo chao hicho.
Aliongeza pia makubaliano hayo yalipitia kwanza Mamlaka ya Udhibiti wa Umeme na Maji (EWURA) na baada ya kupata baraka zao ndio wakapitisha viwango vilivyoridhiwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga, Reinhardt Swart alisema dhumuni la mkataba huo ni kupanua uzalishaji na kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa saruji nchini.
"Tunafahamu kwamba viwanda vyote vya saruji hutumia umeme mwingi kutoka Tanesco hivyo tumeamua kujenga kituo chetu kidogo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa kuzalisha umeme wa 132/33kv ili kupunguza usumbufu usio wa lazima wakati wa mchakato wa uzalishaji na uendeshaji wa kiwanda cha kuzalisha wa saruji," alisema.
Swart alisema kwamba mkataba huo umekuja wakati ambapo Kampuni ya Saruji Tanga ikijenga kinu chake cha pili cha kutengenezea malighafi ya kuzalishia saruji kitakachopanua uwezo wake wa uzalishaji wa saruji nchini.
Kampuni ya Saruji ya Tanga ambao ni watengenezaji wa bidhaa yake maarufu ya saruji ya Simba, ni ya kwanza kusajiliwa katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).

No comments:
Post a Comment