Shirika la Evangelical Mission SOS International kutoka Sweden, kwa kushirikiana na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Mkoa wa Mbeya, wameandaa tamasha la ishara na miujiza litakalofanyika kwenye Viwanja vya Ruanda Nzovwe.
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Mwenyekiti wa Mkutano huo, Askofu Augostino Dedu alisema wameandaa mkutano huo ili kuwaunganisha wakazi wa Mbeya na vitongoji vyake kushiriki sherehe hiyo ambayo huwa haina ubaguzi wa madhehebu yoyote.
Askofu Dedu alisema kama inavyofahamika Mkoa wa Mbeya ndio wenye madhehebu mengi, hivyo kwa kutumia fursa hiyo, wote wanaombwa kushiriki sherehe hizo za ishara na miujiza kwa kila mmoja, itakayohubiriwa na mhubiri maarufu duniani, Mwinjilisti Johannes Amritizer kutoka Sweden.
Alisema mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Julai 9 hadi 13 mwaka huu, kuunga mkono juhudi za Serikali za utii wa sheria bila shuruti.
Mwinjilisti Johannes Amritzer ni mwasisi na Rais wa Shirika la Evangelical Mission SOS International kutoka Sweden na kwa Tanzania, amewahi kutikisa katika miji ya Dar es Salaam, Tanga, Moshi na Mwanza na huduma yake ya SOS imewahi kuchimba visima katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Mbali na hilo, Mkoa wa Mbeya utapata neema ya kutembelewa na wageni wapatao 200 kutoka Marekani na Sweden ambao pia watahudumu kwenye mkutano huo na kufanya uinjilisti katika maeneo mbalimbali yaliyoteuliwa jijini Mbeya na vitongoji vyake.
Katika viwanja vya Ruanda Nzovwe, waimbaji mbalimbali maarufu kutoka nje na ndani ya nchi watamsifu na kumwabudu Mungu. Hiyo ni pamoja na bendi ya huduma ya SOS kutoka Sweden, kundi maalumu la pamoja la kusifu na kuabudu litakalojumuisha waimbaji kutoka madhahebu mbalimbali.
Wengine ni Amani Mwasote, Debora Mwaisabila, Martha Baraka, Tumaini Mbembela pamoja na kwaya mbalimbali.

No comments:
Post a Comment