Friday, July 18, 2014

KAMANDI YA ANGA KUADHIMISHA MIAKA 32 TANGU KUASISIWA

Kamandi ya Jeshi la Anga linatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 32 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1982.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Kamandi hiyo, Meja Jenerali Joseph Kapwani wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Alisema maadimisho hayo yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Julai 23 hadi Julai 28 mwaka huu, na ni ya kwanza tangu kuanzishwa kwa kamandi ya Jeshi la Anga nchini.
Aliongeza kuwa madhumuni ya maadhimisho hayo ni kujitathimini kiutendaji ndani ya kamandi, na kutoa fursa kwa wananchi wa  kanda ya ziwa na taifa kwa ujumla kuona zana mbalimbali zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya ulinzi imara wa anga la Taifa letu.
Alisema Kamandi hiyo ni moja kati ya kamandi tatu ikiwemo ya Jeshi la Nchikavu na Majini, zinazounda Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

No comments: