Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amesema jeshi hilo lina uhakika wa kuwapata watuhumiwa wa mabomu mkoani Arusha na kwingineko nchini, pamoja na kudhibiti matukio hayo baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa taarifa walizopata.
Mangu alisema hayo jana wakati wa mkutano baina yake na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga ambaye ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu milipuko ya mabomu ya Arusha na hali ya usalama nchini kwa sasa, Mangu alisema hali ya usalama siyo ya kutisha kutokana na matukio hayo mapya na ambayo hayajazoeleka nchini.
“Kila tukio lina sababu zake hivyo wanaendelea na uchunguzi wa taarifa walizopata ambazo wanazifanyia kazi na kuna uhakika wa kukabiliana na matukio hayo kwa kuwapata wahalifu na kuyadhibiti kabisa,” alisema IGP.
Huku akiwataka wananchi kushirikiana na polisi kuhakikisha wanafikia malengo hayo mapema kutokana na ukweli kuwa kuna wananchi wanafahamu mipango hiyo na wanaojihusisha, kwani wapo kwenye jamii lakini wako kimya.
Wakati Mangu anaeleza hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amewataka wananchi, viongozi wa taasisi mbalimbali za kijamii, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na viongozi wa dini kushirikiana na serikali ili kuharakisha kasi ya kuwapata watu wanaojihusisha na ulipuaji wa mabomu mkoani Arusha.
Mulongo aliyasema hayo juzi alipokuwa akiahirisha kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), na kusisitiza kuwa serikali haitaki kuona wananchi wasiokuwa na hatia wakipoteza maisha kutokana na matukio ya wachache ambao wanataka kuvuruga amani na utulivu.
Alisema kuwa matukio hayo haelewi ni kwa nini mkoa wa Arusha na Zanzibar zinalengwa kwa mabomu na kueleza kuwa wapo watu ambao wanatengeneza kizazi ambacho hakitaki amani.
Akawataka wananchi wasikalie taarifa za kuwepo watu wenye mabomu, bali waisaidie serikali kuwafichua kwa sababu wapo miongoni mwa jamii wanayoishi nao.
"Leo angalia matokeo yake, wanaofanya matukio haya wanatoka wapi kama sio miongoni mwetu, kila kiongozi aliapa kuilinda amani na wananchi hivyo timizeni wajibu wenu ili wahusika wanaofanya haya waweze kuchukuliwa hatua,’’ alisema.
Tangu mwaka huu kuanza kumetokea zaidi ya matukio matatu ya bomu mkoani Arusha, yakiwemo ya Aprili ambapo watu kadhaa walijeruhiwa na mmoja Sudi Ramadhan alipoteza maisha baada ya bomu kurushwa kwenye baa ya Night Park iliyopo Mianzini.
Pia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Taasisi ya Kiislamu ya Answar Muslim Youth centre, Shehe Soud Ally Soud alijeruhiwa kwa bomu akiwa na mgeni wake kutoka Kenya, Shehe Muhaji Hussein Kifea wakati wakila daku nyumbani kwake eneo la Majengo. Kifea amevunjwa miguu yote miwili na kupoteza vidole vitatu vya mguu wa kulia.
Pia watu wengine wanne wenye asili ya Asia wamejeruhiwa kwa bomu akiwemo mmoja aliyepoteza mguu wakati bomu lilipovurumushwa kwenye mgahawa wa Vama Traditional Indian Cuisine.
Akizungumzia ziara ya Mwenyekiti huyo wa SARPCCO, Mangu alisema Ndeitunga yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa maazimio ya nchi za ukanda huo, kuhusu kukabiliana na uhalifu wa mipakani kama usafirishaji dawa za kulevya, wizi wa magari, ugaidi na mwingineo.
Akizungumzia mafanikio yake akiwa Mwenyekiti wa ukanda huo, Ndeitunga alisema hana shaka ya kuwa Tanzania itakuwa imetekeleza vema udhibiti wa uhalifu mipakani.
Ndeitunga alisema katika ukanda huo wanasisitiza usawa wa kijinsia katika ngazi za maamuzi za polisi ambapo lengo ni kufikia asilimia 50 kwa asilimia 50, jambo ambalo linachukua muda huku kila nchi ikitakiwa kusimamia malengo hayo.
Lakini alisema katika kuhakikisha wanafanikiwa kudhibiti uhalifu katika ukanda huo, Polisi ni wachache na hawako kila sehemu lakini wananchi wa nchi zote wako kila mahali na rahisi kusaidia polisi kudhibiti hali hiyo.
“Tatizo kubwa katika ukanda huu ni dawa za kulevya kwa mabara mengine kuingiza dawa kwetu, hivyo tunahitaji msaada wa kifedha ili kukabiliana na biashara hii ili kutuwezesha katika upelelezi, mafunzo na vifaa huku viongozi wa dini, mila, siasa na wengineo kuhamasisha jamii kuhusu madhara ya dawa hizo kama ukimwi,” alisema.
Alisema changamoto kubwa inatokana na ukosefu wa vifaa vya kutambua dawa hizo, mafunzo kwa polisi pamoja na msaada wa jamii ya kila nchi na kucha kuwa wasikilizaji wa tatizo.
Alisema katika uongozi wake wamefanikiwa katika operesheni kubwa iliyojulikana kama Operesheni Usalama ambayo ilijumuisha umoja wa SARPCCO na ule wa Afrika Mashariki EAPCCO, operesheni ambayo ilileta manufaa makubwa katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka huku akiwa na malengo ya kuendesha operesheni na ukanda mwingine.
Ndeitunga aliyepokea uenyekiti wake kutoka Tanzania, baada ya kumaliza ziara nchini ataelekea Malawi kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hiyo na Septemba mwaka huu atamaliza uenyekiti wake na kuukabidhi kwa mkuu wa Polisi nchini Lesotho.

No comments:
Post a Comment