Lita 400 za damu zinatarajiwa kukusanywa na Benki ya Damu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kutoka kwa wachungaji 800 wanaounda Baraza la Waangalizi la Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG).
Wachungaji hao watachangia damu kwa hiari Julai 10 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya mchango wao wa kijamii katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Jubilee ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Kanisa hilo nchini, yatakayofanyika Julai 13 mwaka huu.
Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Barnabas Mtokambali, alitoa ahadi hiyo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa huduma ya kijamii ya utoaji wa vyandarua 8,550, vitakavyogawiwa katika mikoa ya Mbeya, Rukwa na Njombe.
Askofu Mtokambali alisema uchangiaji damu, utafanyika katika Chuo cha Biblia cha TAG kilichopo Itende jijini Mbeya, na taratibu zote za mawasiliano na Ofisi ya Kanda ya Damu Salama, zimekamilika.
“Ni matarajio yetu wataalamu wa afya kutoka kitengo hiki watafika chuoni hapa wakiwa na vifaa vyao tayari kwa ajili ya kazi hiyo,” alisema Askofu Mtokambali.
Askofu huyo alisema iwapo itabainika kuwepo na uhitaji zaidi wa damu, hamasa itafanyika kwa wageni wengine mbalimbali wapatao 600, ili wachangie damu kwa hiari kabla ya siku ya kilele cha maadhimisho ya Jubilee.
Aliwataka watumishi wa Benki ya Damu Salama, kujipanga ipasavyo kwa kuimarisha vitendea kazi vyao, ikiwemo vifungashio vya damu, ili kumudu uhifadhi wa kiwango kikubwa cha damu kinachotarajiwa kukusanywa kwa wakati mmoja.
Alisema wachungaji kuchangia damu ni sehemu ya kujitoa kuokoa uhai wa wanadamu wenzao kupitia kaulimbiu ya ‘Mungu anaipenda roho yako, anaupenda mwili wako jenga mahusiano naye.’
Kwa mujibu wa Askofu Mtokambali, wachungaji wanaweza kuiga mfano wa Yesu Kristo aliyemwaga damu nyingi msalabani ili kuokoa wanadamu, hivyo na wao kuchangia damu lengo ni kuokoa miili ya wanadamu wenzao, ambao wakiendelea kuishi, wanaweza kulisikia neno la Mungu na hatimaye kupata wokovu wa kiroho.
Akitoa shukrani za Serikali kwa ahadi hiyo na kupokea vyandarua 4,150 kwa ajili ya Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Mkoa huo, Abbas Kandoro alipongeza uongozi wa Kanisa hilo kwa kuonesha moyo wa kuwajali wagonjwa bila kujali tofauti za dini na madhehebu.

No comments:
Post a Comment