Saturday, July 5, 2014

ABIRIA 60 WANUSURIKA KIFO AJALI YA IGUNGA

Abiria 60 wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi katika kijiji cha Makomero wilayani Igunga mkoani Tabora  juzi.
Akizungumza na waandishi wa habari,  Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 10 jioni.
Kamanda Suzan alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Super Sami lenye namba T 835 likitokea mkoani Iringa kuelekea Jijini Jiji la Mwanza.
Ilielezwa kuwa ingawa hakuna aliyekufa wapo waliojeruhiwa vibaya akiwemo kondakta wa basi hilo ambaye aligandamizwa na mlango.

No comments: