jijini Dar es Salaam, zinatarajiwa kunufaika na msaada wa mradi wa
kisima
cha maji uliotolewa na Kampuni ya Bia nchini
(TBL) .
Akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha Sh milioni 29 kwa ajili
ya uchimbaji wa kisima hicho juzi, Mwenyekiti
wa Mtaa wa King’ong'o
Demetrius Mapesi alisema msaada huo
utapunguza uhaba wa maji, unaokabili eneo hilo la Kimara.
Alisema hivi sasa wakazi wa eneo hilo, wanalazimika kununua
maji kwa Sh 500 kwa ndoo moja kutokana na tatizo hilo.
Alisema baada ya kisima hicho, kukamilika
watanunua ndoo moja kwa Sh 100, jambo
alilosema ni sawa na faraja kwao,
kutokana na hali ya uchumi ilivyo.
Hata hivyo, aliwaomba wadau wengine
kujitokeza kutoa msaada zaidi hususani katika eneo la huduma hiyo ya maji
katika mtaa huo, unaokadiriwa
kuwa na wakazi zaidi ya 116,000.
Alisema pamoja na uwepo wa visima vingine
viwili kutoka kwa wafadhili
wengine (Dawasa), bado wananchi wamekuwa
wakilazimika kununua maji kutoka kwa wasambazaji binafsi wanaotumia malori.
Awali, akikabidhi mfano wa hundi hiyo, Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu
alisema: “Kampuni imeguswa na tatizo
linalowakabili wakazi wa eneo hili kwa
muda mrefu na kuamua kuirejeshea jamii sehemu
ya kile inachokipata na
kusaidia jamii.
Mhandisi Onesmo Sigalla kutoka Kampuni ya MO Resources Limited,
alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika katika wiki
tatu na aliwataka wananchi kukitunza kisima hicho kitakapokamilika.

No comments:
Post a Comment