Serikali za
mitaa zitaruhusiwa kuanza kuajiri watumishi wa baadhi ya kada za chini katika
mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Akihojiwa
katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja,
Dar es Salaam, Msemaji wa Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa
Umma, Riziki Abraham, alithibitisha kuwa
Sekretarieti hiyo itakasimu sehemu ya madaraka yake ya kuendesha mchakato wa
jira serikalini kwa serikali za mitaa.
“Sekretarieti
ya Ajira imeandaa mpango wa kukasimisha madaraka yake ya kuendesha mchakato wa
ajira serikalini kwa baadhi ya kada za chini (operation staff) kwenye mamlaka
za Serikali za Mitaa na mchakato huo utaanza mwaka wa fedha 2014/15” alisema.
Pia, alisema
katika kila nafasi ya kazi inayotangazwa kwa waombaji, Sekretarieti hiyo
haizingatii GPA (kiwango cha ufaulu kwa masomo yote ). Alieleza kuwa zipo kada,
ambazo GPA inazingatiwa ;na zipo kada ambazo kinachoangaliwa ni ufaulu tu wa
kawaida na sifa zilizoainishwa.
“Zipo baadhi
ya kada ambazo masharti yake ni pamoja na kuwa na GPA ya kiwango fulani. Kada
ambazo ni lazima GPA kuangaliwa ni kama vile kada za wakufunzi wa vyuo
mbalimbali. Kazi nyingine hazina masharti ya GPA, kinachoangaliwa ni ufaulu tu
na sifa zilizoainishwa katika tangazo la nafasi za kazi kulingana na kada husika”,
alisema Riziki.
Alitaja moja ya matatizo wanayopata
waombaji wa kazi kuwa ni kupotelewa na vyeti vya kitaaluma. Alisema waombaji wa
kazi ambao wamepata tatizo hilo, wanachopaswa kufanya ni kuripoti kwenye
mamlaka husika, alikokuwa amepata cheti hicho ili apewe mwongozo wa kufanya na
kutangaza kupotelewa kwa cheti au vyeti kwenye chombo cha habari (gazeti). “Ikithibitika hivyo mamlaka
husika kwa mfano Baraza la Mitihani wana utaratibu wa kuwasiliana na
Sekretarieti ya Ajira kwa kutoa majina ya watu waliopoteza vyeti na hatimaye
huruhusiwa kufanya usaili” alisema.

No comments:
Post a Comment