Mwili wa nguli katika tasnia ya habari, Nkwabi Ng'wanakilala unatarajia kuwasili leo jioni kutokea hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, na kuzikwa kesho shambani kwake Kibamba CCM, jijini Dar es Salaam.
Ng'wanakilala ambaye hadi mauti yanamkuta alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), alifariki juzi usiku wa kuamkia Jumamosi katika hospitali ya Bugando.
Akizungumza na HabariLeo kuhusiana na taratibu za mazishi, mtoto wa marehemu, Fumbuka Ng'wanakilala, alisema mwili wa mwanahabari huyo, utawasili leo jioni na kesho utazikwa shambani kwake.
"Wanandugu tuko huku shambani kwake tukiendelea na taratibu nyinginezo za mazishi ili kuhakikisha tunauhifadhi mwili wa mzee," alisema Fumbuka na kuongeza kuwa Misa kwa ajili ya mazishi itafanyikia hapo hapo shambani kabla ya kuzika.
Wakati wa uhai wake, Ng'wanakilala aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Radio Tanzania Dar es salaam (RTD),sasa TBC na lililokuwa Shirika la Habari Tanzania (Shihata).
Kadhalika wakati wa uhai wake alifanya kazi katika tasnia ya habari na kushiriki katika masuala mbalimbali ya habari kama mhadhiri, mtafiti, mshauri na mwandishi na mchapishaji binafsi wa vitanu ma majarida mbalimbali.

No comments:
Post a Comment