Mjamzito Agatha Isack (19) amekufa kwa kipigo kutoka kwa mumewe akisaidiwa na mwanamke anayeaminika kuwa hawara yake, akimtuhumu kuwa mvivu wa kulima shambani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha kifo hicho na kuongeza kuwa mama huyo mjamzito ambaye ni mkazi wa kijiji cha Manga, Kata ya Kasokola wilayani Mlele alifikwa na umauti akikimbizwa katika zahanati kijijini hapo kwa matibabu.
Inadaiwa baada ya hali yake kubadilika ghafla kutokana na kipigo kutoka kwa mumewe Vitus Mlengo (23), mume alikodisha pikipiki na kumkimbiza kwenye zahanati, lakini alikata roho akiwa njiani.
Akielezea mkasa huo unaodaiwa kutokea juzi saa sita mchana nyumbani kwa wanandoa hao kijijini humo, Kamanda Kidavashari alisema awali baada ya kipigo mwanamke huyo alikwenda katika zahanati iliyopo kijijini humo kwa uchunguzi zaidi na matibabu.
Kabla ya kufika hospitalini alikwenda kwa mama yake mdogo aitwae Anastazia Charles na kumsimulia jinsi alivyopigwa na mumewe akishirikiana na Faustina Matheo (31) ambaye anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mlengo.
“Baada ya kutibiwa Agatha alipitia nyumbani kwa bibi yake kijijini humo na kumweleza jinsi alivyopigwa na mumewe pia alimfahamisha bibi yake kuwa mumewe alimuonya asirudi nyumbani bila mboga hivyo bibi yake huyo alimpatia mboga naye akarejea kwake,“ alibainisha Kamanda Kidavashari.
Inadaiwa alipofika nyumbani kwa mumewe, Mlengo alimfukuza ndipo alirudi kwa bibi yake na kulazimika kulala nyumbani kwake hadi asubuhi ya siku iliyofuata ambapo Agatha alifuatana na bibi yake huyo ndipo mumewe akakubali kumpokea .
Kidavashari alifafanua kuwa juzi, saa mbili usiku Agatha alishindwa kula chakula alichokipika mwenyewe akilalamikia kuhisi maumivu makali kichwani ndipo mumewe alipoona hali yake imebadilika ndipo alilazimika kuomba msaada wa pikipiki kwa rafiki yake aitwae Alfred Kasonso na kumkimbiza katika zahanati kijijini humo kwa matibabu .
Kamanda alithibitisha kuwa mume wa marehemu huyo na Faustina wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Katika tukio lingine, mwendesha pikipiki ‘bodaboda', Daniel Kapufi (20) mkazi wa mjini Sumbawanga mkoani Rukwa ameuawa kikatili kwa kukatwa katwa na shoka na mapanga baada ya ‘kunaswa’ akisafirisha nyama ya ng’ombe inayodaiwa kuwa ya wizi akitumia pikipiki yake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana saa tisa usiku katika kitongoji cha Malangali, Manispaa ya Sumbawanga.
Mtendaji wa Kata ya Malangali, Basil Stima, alisema kuwa chanzo cha kijana huyo kuuawa ni kutokana na kunaswa akisafirisha nyama ya ng'ombe kwa kutumia usafiri wa pikipiki yake, ng’ombe anayedaiwa kuibwa na kuchinjwa katika msitu karibu na kitongoji hicho cha Malangali.
Alisema kuwa baada ya bodaboda huyo kubeba furushi la kwanza la nyama hiyo, alirudia mzigo wa pili ndipo aliponaswa na kundi la watu ambao walimhoji alikoitoa nyama hiyo ambapo wakati akijieleza ghafla walianza kumshushia kupigo huku wakitumia silaha mbalimbali ya jadi, yakiwemo mapanga na kumsababishia umauti kisha wakaichoma moto pikipiki yake.

No comments:
Post a Comment