Sunday, April 13, 2014

WEZI 15 WAVAMIA NA KUUA KIBABU CHA MIAKA 60

Mkazi mmoja wa Chang'ombe jijini Dar es Salaam ameuawa na wezi waliovamia nyumbani kwake baada ya kupigwa mapanga wakimtaka awapatie fedha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 8:00 usiku katika eneo la Machimbo Mwisho ambapo wezi wapatao 15 walivamia nyumbani kwa Vedastus Selema (60) na kumshambulia kwa mabapa ya upanga wakimtaka awape fedha.
Kamanda Kiondo alisema Selema alipelekwa hospitali ambako alifariki wakati akihudumiwa. Hata hivyo hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusika na tukio hilo.
Katika tukio jingine eneo la Sinza Kumekucha jijini Dar es Salaam, watu wawili wanaume wasiofahamika wanaokadiriwa kuwa na miaka 25 na 30 wameshambuliwa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kupigwa kwa kutuhumiwa kuwa ni wezi. Walifariki wakati wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Sinza Palestina.
Aidha tukio jingine katika duka la kuchezesha kamari lililoko eneo la Tandale walivamia watu watatu ambao walimfunga kwa kamba Maria Samson na kupora Sh 396,000 na simu mbili za mkononi. Upelelezi unaendelea.

No comments: