Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, ipo katika hatua za mwisho kufungua kiwanda cha chanjo ya mifugo cha Kibaha cha mkoani Pwani huku ikiwataka wananchi kuongeza kasi ya uzalishaji wa kuku ili kukabiliana na ukuaji wa soko la bidhaa hiyo ambalo kwa sasa linakua kwa kasi nchini.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Wizara hiyo, Dk Titus Kamani wakati wa warsha ya siku moja iliyowahusisha viongozi wa wizara hiyo, wazalishaji, wafanyabiashara na wadau wengine kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo na hivyo kukwamisha ukuaji wake.
Alisema katika kuhakikisha maendeleo ya sekta hiyo yanakuwa kwa haraka ili kuleta tija kwa wananchi wake, Serikali imeanza kukifanyia maboresho kiwanda cha chanjo cha Kibaha ambacho awali kilifungwa na baadhi ya watendaji wake kuchukuliwa hatua kutokana na uzalishaji wa chanjo bandia na zilizo chini ya kiwango na hivyo kusababisha athari kwa wafugaji.
"Matumaini kiwanda hiki kitafunguliwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo mara baada ya kukamilika kwa taratibu mbalimbali ikuhusisha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambao hivi karibuni tuliwataka waende kujiridhisha ili tuweze kuanza uzalishaji," alisema Dk Kamani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa uendelezaji wa mazao ya mifugo kutoka katika Wizara hiyo, Dk Yakobo Missanga alisema changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni pamoja na upatikanaji wa vifaranga vyenye ubora na hasa vya nyama, hali inayosababisha thamani ya kuku kushuka pamoja na chakula cha kuku chenye ubora wa kutosha.
Naye mmoja wa wazalishaji wa kuku kutoka Kampuni ya 'Mkuza Chicks', Florance Maximambali alisema pamoja na sekta hiyo kuchangia pato la Taifa kwa kiasi kikubwa bado imeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi kutokana na uzalishaji wake kuwa mdogo na hivyo kuiomba Serikali kuisaidia ili ufugaji uweze kuwa wa tija.

No comments:
Post a Comment