Samuel Sitta (kushoto) alipokuwa akikabidhiwa kiti na Pandu Ameir Kificho. |
Akiwa ndiyo kwanza ametoka kuapishwa na kuanza kazi, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta amepingwa na mjumbe wa bunge hilo, Tundu Lissu kuwa amefanya maamuzi kwa kukiuka kanuni.
Ukiukaji huo umedaiwa kuwapo kwenye tangazo lake kuwa Rais Jakaya Kikwete atalihutubia Bunge baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuwasilisha rasimu ya Katiba bungeni.
Akiomba mwongozo, Lissu alisema kuwa Kanuni inamtaka Rais Jakaya Kikwete kulihutubia Bunge kwanza kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuwasilisha rasimu ya Katiba bungeni.
Alitaka mwongozo wa Mwenyekiti kuhusu tangazo lake hilo alilolitoa juzi kabla ya kuanza kuwaapisha wajumbe wa bunge hilo akieleza kwamba Jaji Warioba atalihutubia Bunge kesho na Rais anatarajiwa kulihutubia Bunge Jumanne au Jumatano.
“Mwenyekiti naomba mwongozo wako kuhusu tangazo lako kwamba Jaji Warioba atakuja kuwasilisha rasimu yake ndipo Rais aje kulihutubia Bunge, kanuni zetu zinamtaka Rais aje kwanza kulihutubia Bunge ndipo Jaji Warioba aje kuwasilisha rasimu yake.”
“Tuliamua hivi kwa kuwa tuliona iwapo Jaji Warioba akitangulia kuwasilisha rasimu baada ya hapo ndipo Rais aje kulihutubia Bunge itaonekana kama vile Rais Kikwete amekuja kumjibu Mwenyekiti wa Tume,” alisema.
Lissu ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kanuni alihoji pia kanuni aliyoitumia Mwenyekiti huyo kuruhusu mjadala wa jumla wa muda wa siku tatu kabla ya wajumbe kuanza kazi za kamati.
Alisema kwa mujibu wa kanuni hizo, kazi ya kwanza inayotakiwa kufanywa na wajumbe inaanzia katika kamati zitakazoundwa na kuhoji Sitta ametumia kanuni ipi kuruhusu mjadala wa siku tatu.
Akijibu hoja hizo za Lissu, Sitta alisema Rais hawezi kuja kulihutubia Bunge wakati hakuna ajenda yoyote ambayo imewasilishwa kwa wajumbe hadi sasa na kusisitiza; “ Kwa uzoefu wangu katika Bunge lazima kwanza tuwe na ajenda, Jaji Warioba atakuja kuwasilisha rasimu ili tuwe na ajenda mkononi ndipo Rais aje kulihutubia Bunge.
“Tumelijadili hili na wenzangu tumeona iwe hivyo ikiwezekana tutatengua kanuni kumruhusu Jaji Warioba kuwasilisha kwanza Rasimu ya Katiba kwa wajumbe”.
Sitta alisema kanuni zinamruhusu kutumia busara yake kuamua baadhi ya mambo kwa namna anavyoona inafaa hivyo ametumia madaraka yake kuamua hivyo ili wajumbe wawe na mjadala mpana kabla ya kwenda kwenye kamati.
“Katika kipindi hiki pia nitapata muda wa kuwajua wabunge na hivyo kuweza kuwapanga katika kamati mbalimbali, wajumbe zaidi ya 600 mliopo humu ni wengi lazima nipate muda wa kutafakari kabla ya kuunda kamati,” alisema.

No comments:
Post a Comment