Basi likiteketea barabarani mkoani Singida. |
Watu 129 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 299 kujeruhiwa kutokana na ajali mbalimbali za barabarani, zilizotokea katika kipindi cha mwaka mmoja mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema hayo juzi katika taarifa yake.
Alisema kuwa ajali zilizoripotiwa mwaka jana zilikuwa 246, ikiwa ni ongezeko la ajali mbili tu, ikilinganishwa na idadi ya mwaka juzi.
Kamwela alisema mwaka jana watu 129 walipoteza maisha na wengine 299 walijeruhiwa. Alisema sababu za kutokea ajali hizo ni ongezeko la vyombo vya usafiri hasa pikipiki maarufu kama bodaboda na bajaj.
Sababu nyingine ni matumizi mabaya ya barabara, uzembe wa madereva, mwendo kasi na kutokuzingatia kikamilifu sheria za usalama barabarani.
Katika kipindi hicho, jumla ya makosa madogo madogo 22,584 yaliripotiwa ambapo watu 20,127 walikamatwa kwa makosa mbalimbali yanayohusu ukiukaji wa sheria za usalama barabarani.
Alieleza kuwa kutokana na makosa hayo, Sh milioni 684.9 zilikusanywa na jeshi hilo kwa njia ya tozo ya adhabu, ikiwa ni ongezeko la Sh milioni 185.1, sawa na asilimia 37 ikilinganishwa na makusanyo yote ya tozo kwa mwaka juzi.

No comments:
Post a Comment