Picha mbalimbali za mabaki ya gari dogo walilokuwamo polisi hao. |
Ajali hiyo iliyotokea jana majira ya saa 8.45 usiku wa manane katika kijiji cha Mtumba wilayani Kongwa ilihusisha basi la kampuni ya Mohamed Trans lenye namba za usajili T 997 AVW lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma ambalo liligongana na gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T770 ABT.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema ajali hiyo ilisababisha vifo vya askari hao watano wanaofanyia kazi wilayani Kongwa ambao walikuwa wakitokea kwenye sherehe ya kuwaaga wastaafu wa jeshi hilo iliyofanyika kwenye bwalo la Chuo cha Mipango.
Wote ni askari Polisi wa Wilaya ya Kongwa na kwamba hakuna abiria aliyeumia katika basi.
Alisema mara baada ya kugongana, basi hilo liliikokota gari hiyo ndogo umbali wa mita takribani 50 na kisha basi hilo kuendelea kuserereka tena umbali wa takribani mita 100 kabla ya kusimama.
Misime aliwataja askari hao waliopoteza maisha kuwa ni D.9084 D/CPL. Adolph S/O Meshack Silla mwenye miaka 51 (Mgogo), F.6459 D/C. Evarist S/O Moses Bukombe, mwenye miaka 34 (Muha), H.3783 PC. Deogratius S/O Patrick Mahinyila mwenye miaka 29 (Mgogo), WP.10337 PC. Jackline D/O Augustine Tesha mwenye miaka 22 (Mchagga) na WP.10382 PC. Jema D/O Jimmy Luvinga mwenye miaka 20 (Mhehe).
No comments:
Post a Comment