Dk. Sengondo Mvungi mara baada ya shambulio hilo lililochukua uhai wake. |
Familia ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi imesema asitafutwe mchawi katika kifo cha ndugu yao huyo.
Tamko hili lilitolewa katika misa takatifu ya kumuombea marehemu Mvungi iliyosomwa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam jana ambapo pia Chama cha NCCR Mageuzi kilisema kimewasamehe wabaya wa Dk Mvungi.
Padri aliyekuwa akiendesha misa hiyo, Gallen Mvungi ambaye ni mtoto wa kaka wa Dk Mvungi alisema mambo mengi yamesemwa katika kipindi cha msiba na mpaka sasa lakini katika kifo cha mpendwa wao asitafutwe mchawi.
"Tusishikane mashati, tusimtafute mbaya ni nani aliyechukua maisha ya Dk Mvungi na pia tusitafute mchawi nani, Dk Mvungi aliishi maisha ya kumpendeza Mungu na sasa Mungu amemwita baada ya kuupendezesha ulimwengu," alisema Pande Mvungi.
Alisema Mungu amefanya haraka kumuondoa ili uovu, fitna, chuki, visiweze kumuondolea nia yake ya kufika mbinguni na kwamba Dk Mvungi alikuwa ni mshumaa katika taifa hivyo asiondoke na amani yake taifa likaingia katika vurugu.
Mbunge wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema kwa niaba ya chama na pia familia hawana adui yeyote na kwamba wale waliokuwa na chuki na fikra potofu dhidi ya Dk Mvungi wamewasamehe.
"Katika kipindi hiki tumesikia na kuona mambo mengi, kwa niaba ya Chama na pia nazungumza kwa niaba ya familia, tumewasamehe wote, tumemtoa Dk Mvungi kama sadaka kwa Watanzania na pia taifa kwa ujumla."
"Wale waliokuwa na chuki na fikra potofu tumewasamehe kama familia naongea na sasa tunaishi katika imani tunaamini aliyotufundisha mpendwa wetu Dk Mvungi tunaanza maisha mapya tunasonga mbele na tunamuenzi kwa kuhakikisha tunapata Katiba mpya," alisema Mbatia.
Mtoto wa marehemu Dk Mvungi, Dk Natujwa Mvungi alisema baba yake ni mtu ambaye alikuwa akiipenda nchi kwa moyo wake wote na katika maisha yake alikuwa akifikiri ni namna gani Tanzania itainuliwa na watu wake waishi katika maisha bora.
"Katika miaka 20 hiyo hasa mambo ambayo baba yetu alikuwa anayazungumza kila siku hasa ni elimu bora kwa Watanzania, akifikiria kuanzisha Chuo cha Bagamoyo na kiu yake kukamilika akiona Katiba mpya," alisema Dk Natujwa.
Dk Natuja ambaye ni daktari wa falsafa katika sheria, alisema wanamshukuru Rais Jakaya Kikwete kutimiza ndoto yake hiyo kwa kumpa nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika maandalizi ya Katiba kwa kumteua kuwa mjumbe katika Tume ya Katiba na kwamba urithi wa taaluma aliowaachia watoto wataendeleza yale aliyoyaacha.
Katika misa hiyo familia ilitoa jembe, panga, msumeno, mbuzi, kuonesha Dk Mvungi alikuwa mtu wa kawaida na pia kalamu na vitabu, mbali na zawadi hiyo walitoa pia maneno yaliyowekwa kwenye fremu ambayo yalikuwa ni wimbo wake wa kila siku yaliyosomeka 'Katiba ni Tendo la Maridhiano'.

No comments:
Post a Comment