Barabara ya Uhuru eneo la Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. |
Usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam kuwa njia nne, umekamilika ili kuondoa msongamano wa magari katika barabara hiyo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge aliliambia Bunge jana kuwa serikali kwa sasa inatafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo, unaolenga kupunguza msongamano wa magari jijini.
Lwenge alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (CCM) aliyehoji kwa nini serikali haitoi kipaumbele kwa barabara ya Uhuru kwa kuitengea fedha ili itengenezwe, kutokana na kuwa na hali mbaya na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.
Akijibu swali hilo, Lwenge alisema katika mwaka wafedha 2012/ 2013, Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Taifa wa Barabara (TANROADS) ilitumia Sh bilioni 1.325 za Mfuko wa Barabara, kufanya matengenezo maalumu katika barabara ya Uhuru.
Aidha, alisema katika mwaka huu wa fedha Sh milioni 500 kutoka Mfuko wa Barabara na Sh milioni 407 zikiwa ni fedha za maendeleo, zimetengwa kwa ajili ya matengenezo maalum ya sehemu korofi.
Alisema zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi zimetangazwa upya Oktoba mwaka huu baada ya uchambuzi wa zabuni za awali kushindwa kutoa Mkandarasi anayefaa kwa kazi za matengenezo.

No comments:
Post a Comment