Friday, November 1, 2013

FAMILIA YAISHI NA MAITI KWA MIEZI 10 NDANI YA NYUMBA ILI KUFUKUZA MAPEPO...

Mji wa Ramavarma Puram ambako familia hiyo inaishi.
Familia moja ya kishirikina imeweka mwili wa ndugu yao aliyekufa kwenye nyumba yao kwa miezi 10 ili kufukuza mapepo.

Wanafamilia watatu wa familia hiyo walikutwa wakiishi na mwili huo ulioharibika vibaya wa ndugu yao wa kike katika nyumba yao huko Nagercoil, India.
Baaday ya jirani mmoja kulalamikia kuhusu harufu hiyo mbaya kutoka kwenye nyumba hiyo iliyoko Ramavarma Puram, polisi walikuta mwili huo wa Umadevi mwenye umri wa miaka 56 ukiwa umefunikwa na shuka kwenye moja ya vyumba hivyo. alifariki Desemba 3, 2012.
Mtoto wa kiume wa marehemu huyo, mama yake na kaka yake, walilazwa katika hospitali ya serikali kwa hofu kwamba wanaweza kuwa wameambukizwa na matatizo ya kiakili, imeripotiwa.
Polisi walisema mama wa Umadevi, Sarojini, mtoto wake wa kiume Sivaraman na kaka yake Sellampillai mara zote walikuwa wakifunga nyumba yao na kutozungumza na majirani.
Walikuwa wakiishi kwenye nyumba ya pensheni ya mume wa Sarojini, Subramaniam Pillai. Wakati Sarojini hakutokea kulipia cheti cha maisha, hawakuweza kupata pensheni hiyo katika miezi ya hivi karibuni.
Polisi walihisi mwili huo ulikuwa ukihifadhiwa ndani ya nyumba sababu hawakuwa wakiweza kulipia gharama za uchomaji moto mwili huo lakini kisha maofisa walihisi wanaweza kuwa hawakuwa sawa.
"Wote watatu walionekana kama walikuwa na matatizo ya kiakili. Hiyo ndio moja ya sababu zilizofanya wapelekwe hospitali hapo," ilisema polisi.
Hatahivyo, mhitimu Sellampillai aliwaeleza polisi baba yake alifariki baada ya kuona mzimu kwenye nyumba hiyo na akaweka mwili wa dada yake katika nyumba hiyo ili kuzuia mapepo yasiingie ndani.
"Kaka yangu, Perumal, pia alifariki na sasa dada yangu, Umadevi, amefariki. Kuna mtu alisema kwamba kama kuna mwili wa mfu katika nyumba, kamwe mzimu hauwezi kuja."
Maofisa wa polisi walisema Sellampillai aliongea nao kwa lugha ya Kiingereza fasaha.

No comments: