Friday, November 1, 2013

ABAMBWA AKISAFIRISHA NYOKA KWENYE KASHA LA CHAKULA NDANI YA NDEGE...

Polisi na maofisa wa vikosi vya mpakani walilazimika kukutana kwenye ndege moja iliyokuwa ikiingia nchini Uingereza juzi usiku kufuatia nyoka aliyekuwa akisafirishwa katika ndege hiyo ndani ya kikasha cha kubebea chakula.

Abiria walielezea mshituko wao baada ya nyoka huyo kugunduliwa kwenye ndege ya EasyJet iliyokuwa ikitokea Tel Aviv, Israel, kuelekea Uwanja wa Ndege wa Luton juzi.
Imefahamika mamlaka hizo ziliitwa wakati ndege hiyo bado ikiwa nusu ya safari angani na kusubiria ndege hiyo katika lango la kuingia itue takribani masaa matatu baadaye.
EasyJet inasema watu hao waliokuwa ndani ya ndege hiyo hawakuwa katika hatari lakini imelalamikia Uwanja wa ndege wa Israeli sababu walishindwa kubaini nyoka huyo wakati wa ukaguzi wa usalama.
Sehemu kubwa ya abiria walichukulia ni kichekesho, wakifananisha tukio hilo na filamu maarufu ya Hollywood ya 'Snake on a Plane', ambayo ilichezwa na Samuel L. Jackson.
Tukio la juzi usiku halikuwa zito kihivyo, wakati reptilia huyo alipogundulika kuwa ni nyoka asiye na sumu aliyefichwa ndani ya kikasha cha chakula.
Imefahamika kwamba wafanyakazi wa mpakani walishughulikia na tukio hilo na kumruhusu abiria huyo kuondoka uwanjani hapo na nyoka wake.
EasyJet ilisema jana kwamba nyoka huyo alikutwa ndani ya 'kasha dogo la kubebea chakula'.
"Tunathibitisha kwamba abiria mmoja alipanda na nyoka mdogo, wa kufugwa ndani ya kasha kwenye ndege moja kutoka Tel Aviv kwenda Luton," msemaji mmoja alisema jana.
"Mara baada ya mfanyakazi kubaini hili walishughulikia suala hilo, haraka kwa kuwasiliana na mamlaka kuhakikisha wanaifuata ndege hiyo huko Luton. Usalama wa abiria kila wakati ni kipaumbele chetu cha juu kabisa.
"Nyoka huyo asiye na madhara alibakia kwenye kasha lake wakati wote na abiria hawakuwa kwenye hatari yoyote. Tumewasilisha suala hili na uwanja wa ndege kufahamu kwanini nyoka huyo hakuweza kugundulika wakati wa ukaguzi."
Nyoka sugu, ambao hupatikana zaidi Amerika ya Kaskazini, wanaweza kufikia urefu wa hadi futi 6 na huwinda wanyama wanaojificha kwenye mashimo, kuwaua kwa kuwabana.
Kusita kwao kung'ata huwafanya kuwa wanyama maarufu, na katika utekaji wao wanaweza kuishi hadi umri wa miaka 23.

No comments: